Meneja wa Vodacom, Mkoa wa Kigoma Kashinde Umella (kulia), akisalimiana na Baba mzazi wa mshindi wa shilingi Milioni 100 wa Promosheni ya Vodacom Mahela, Mzee Nicodemus Nalisis, alipofika Uwanja wa ndege kumlaki kijana wake, Valerian Kamugisha (katikati), alipowasili Kigoma mara baada ya kukabidhiwa kitita chake hapo juzi.
Mshindi wa shilingi Milioni 100 wa Promosheni ya Vodacom Mahela, Valerian Kamugisha, akiwaonesha majirani pamoja na baba yake mzazi moja ya picha aliyotolewa kwenye gazeti la Tanzania Daima, jinsi alivyokabidhiwa pesa zake hivi karibuni, mara baada ya kuwasili nyumbani kwao, mkoani Kigoma jana.
Mshindi wa shilingi Milioni 100 wa Promosheni ya Vodacom Mahela, Valerian Kamugisha, akiwaonesha majirani pamoja na baba yake mzazi, moja ya picha aliyotolewa kwenye gazeti la Habari Leo, jinsi alivyokabidhiwa pesa zake hivi karibuni, mara baada ya kuwasili mkoani Kigoma, nyumbani kwao.
Baba mzazi wa Mshindi wa shilingi Milioni 100 wa Promosheni ya Vodacom Mahela, Mzee Nicodemus Nalisis, akiongea machache mara baada ya kijana wake, Kamugisha kuwasili Kigoma.
MZAZI wa kijana aliyeshinda shilingi milioni 100, katika Promosheni ya 'VODACOM MAHELA', Nicodemus Nalisis ametoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Kigoma kujenga tabia ya kushiriki mashindano mbalimbali yanayotolewa na kampuni za simu za mkononi hapa nchini.
Mzee Nicodemus alisema hayo jana katika uwanja wa ndege mkoani Kigoma wakati alipowasili kumpokea kijana wake Valerian Nicodemus Kamugisha aliyewasili mkoani hapa mara baada ya kukabidhiwa kitita chake cha shilingi milioni 100 juma tatu ya wiki hii baada ya kuibuka mshindi wa shindano hilo.
Alisema kuwa hatua ya kushiriki mashindano hayo yatatoa fursa ya ushindi kwa wananchi wengi mkoani Kigoma hivyo kuongeza uwezekano wa Mkoa wa Kigoma kutoa washindi wengi katika mashindano yanayoendeshwa na Vodacom na kupadilisha maisha yao ya kiuchumi na kimaendeleo kiujumla.
Nicodemasi alieleza kufurahishwa na hatua ya mwanae kushinda katika shindano hilo na kwamba, mbali na hiyo kuwa fedha hizo ni msingi mzuri wa maisha ya kijana huyo, lakini pia ushindi huo ni fahari kwa wananchi wa Kigoma na historia kubwa ya kijana huyo na familia.
Alisema kuwa ingawaje yeye, alishiriki katika promosheni hiyo bila mafanikio na mwanae kushinda basi anampongeza kwani sawa sawa kama yeye kashinda tu.
Licha ya kuipongeza Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kwa mashindano mbalimbali likiwemo la VODACOM MAHELA na kwamba hatua hiyo inachangia katika kukuza na kupanda uchumi kwa mwananchi mmoja mmoja na familia kwa ujumla.
Aidha mmoja wa majirani wa familia ya mshindi huyo Bw Jackson Kakwaya mfanyabiashara wa bidhaa madukani alisema hatua ya ushindi wa kijana huyo inapaswa kuwa hamasa tosha kwa watu wengi wa mkoa huu kushiriki katika shindano hilo kikamilifu.
Alisema ushindi huo umemfanya aamini kuwa hakuna upendeleo katika shindano hilo na hakutarajia kama ingewezakana mkazi wa kigoma kushinda shindano tena la fedha nyingi kiasi hicho.
Alisisitiza Vodacom kuendeleza program kama hizo hatua ambayo alisema inawapa fursa washindi kuboresha maisha yao ghafla kutoka katika hali ya chini au ya kawaida nakuwa tajiri kwa muda mfupi.
Hata hivyo Bw Kakwaya alisisitiza umuhimu wa kijana aliyeshinda shindano hilo nakunyakuwa milioni 100, kukaa chini na kupanga mikakati madhubuti itakayo boresha maisha yake na familia badala ya kuzitumia katika anasa.
Kwa upande wake mshindi wa Vodacom Mahela Bw Valerian Kamugisha mbali na kupongeza Vodacom kwa kumkabidhi zawadi hiyo alikiri shindano hilo kutokauwa na mianya yoyote ya rushwa nakusema kuwa hana ndugu katika kampuni hiyo lakini ameshinda.
Aliwataka wananchi kuamini mashindano yanayoendeshwa na Vodacom nakushiriki mara kwa mara jambo ambalo litaongeza idadi ya washindi mkoani Kigoma nakuondoa dhana kuwa Kigoma haiwezi kutoa mshindi ni mwisho wa reli.
“Hakuna aliyeamini kuwa Kigoma ingeweza kutoa mshindi tena mtu kama mimi, lakini ndio hivvo nimeshiriki kikamilifu bila kuchoka hatimaye nimeibuka na milioni 100” alisema Kamugisha.
Kamugisha pamoja na kushinda alisema ataendelea na kushiriki mashindano mengine ya Vodacom ili kupata fursa zaidi kushinda fedha zingine huku akiwashauri wananchi hasa vijana mkoani Kigoma kuchangamkia fursa hizo kujaribu bahati ili kuboresha maisha.
No comments:
Post a Comment