TANGAZO


Tuesday, May 28, 2013

Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal azindua duka la Fenicha la Cleopatra, Pugu Road jijini Dar es Salaam

Duka la thamani la Cleopatra, lililopo Barabara ya Nyerere, maeneo ya Sido, Kipawa ambalo Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, alilizindua juzi. Bidhaa za duka hilo, zimetengenezwa na Kampuni hiyo kutoka nchini Misri. (Picha zote na Kassim Mbarouk wa bayana.blogspot)
Balozi wa Misri nchini Tanzania, Hossam Moharam, akimtambulisha mkewe kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kulia), wakati walipokuwa wakimsubiri Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, awasili kwa ajili ya uzinduzi wa duka hilo.
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Namibia nchini, Japhet Isaack, mara baada ya kuwasili kuzindua duka la fenicha la Cleopatra, Barabara ya Nyerere, Dar es Salaam juzi. Wa pili kushoto ni Balozi wa Angola nchini, Profesa Ambrose Lukoki.
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Oman nchini, Yahya bin Moussa al Bakari katika hafla hiyo.
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akikata utepe ili kuzindua duka la fenicha la Cleopatra.
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, Balozi wa Misri nchini, Hossam Moharam (kulia) na Meneja wa Kanda wa Kampuni ya Cleopatra, Gamal El Feky (kushoto), wakipiga makofi, kufurahia uzinduzi huo.  
Mkurugenzi wa Mradi wa utengenezaji wa thamani wa Kampuni ya Cleopatra Furniture, Muhammad  Al Katawi, akimuonesha Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, jinsi kabati kubwa la nguo, lililotengenezwa na kampuni hiyo, linavyoonekana kwa ndani, wakati alipokuwa akiangalia bidhaa mbalimbali za duka alilolizindua, Barabara ya Nyerere, maeneo ya Sido, Dar es Salaam juzi.
Mkurugenzi wa Mradi wa utengenezaji wa thamani wa Kampuni ya Cleopatra Furniture, Muhammad  Al Katawi (kulia), akimwelezea Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, jinsi meza ya kulia chakula ilivyotengenezwa na kiwanda cha kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa Mradi wa utengenezaji wa thamani wa Kampuni ya Cleopatra Furniture, Muhammad  Al Katawi akimwelezea jambo, Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akiangalia bidhaa kwenye duka la kampuni hiyo, mara baada ya kulizindua duka hilo, jijini Dar es Salaam juzi.
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiangalia moja ya meza iliyotengenezwa kwa kioo na kiwanda cha kamuni hiyo, kilichopo nchini Misri. 
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiwa amekaa kwenye moja ya viti vilivyotengenezwa na kiwanda cha kampuni hiyo, wakati alipofika kulifungua la Cleopatra, Barabara ya Nyerere, maeneo ya Sido, Dar es Salaam juzi.
Mkurugenzi wa Mradi wa utengenezaji wa thamani wa Kampuni ya Cleopatra Furniture, Muhammad Al Katawi (kulia), akimwelezea Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, jinsi moja ya meza za kampuni hiyo, ilivyosanifiwa katika matengenezo yake na kiwanda cha kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa Mradi wa utengenezaji wa thamani wa Kampuni ya Cleopatra Furniture, Muhammad  Al Katawi (chini kulia), akimwelezea Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, jinsi meza anayoiangalia ilivyotengenezwa na kiwanda cha kampuni hiyo, mara baada ya kulifungua la duka la Cleopatra, Barabara ya Nyerere, maeneo ya Sido, Dar es Salaam juzi.
Mkurugenzi wa Mradi wa utengenezaji wa thamani wa Kampuni ya Cleopatra Furniture, Muhammad  Al Katawi (kulia), akimuonesha Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bila, moja ya viti vilivyotengenezwa na kiwanda cha kampuni hiyo, nchini Misri. 
Meneja wa Kanda wa Kampuni ya Cleopatra, Gamal El Feky, akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo, kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, kutoa hotuba yake.
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akitoa hotuba yake kwenye uzinduzi wa duka la Kampuni ya Cleopatra.

No comments:

Post a Comment