TANGAZO


Tuesday, May 28, 2013

Tigo yazindua huduma mpya ya 'Nunua na Uza' kwa Tigo Pesa

Meneja Bidhaa wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, William Mpinga, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, wakati kampuni hiyo, ilipozindua huduma mpya ya 'uza na nunua' kupitia Tigo Pesa. Kulia ni mwakilishi wa Kampuni ya Fronline Porter Novelli, Elias Bandeko.


Meneja Bidhaa wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, William Mpinga, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, wakati kampuni hiyo, ilipozindua huduma mpya ya 'uza na nunua' kupitia Tigo Pesa. Kulia ni mwakilishi wa Kampuni ya Fronline Porter Novelli, Elias Bandeko.


Meneja Bidhaa wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, William Mpinga, akijibu maswali ya waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, wakati kampuni hiyo, ilipozindua huduma mpya ya 'uza na nunua' kupitia Tigo Pesa. Kulia ni mwakilishi wa Kampuni ya Fronline Porter Novelli, Elias Bandeko.


Waandishi wa habari, wakiwa kazini wakati Meneja Bidhaa wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, William Mpinga, akizungumza nao, Dar es Salaam jana, kuhusu uzinduzi wa huduma mpya ya 'uza na nunua' kupitia Tigo Pesa. 

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Tigo Tanzania imezindua huduma nyingine ya kufanya manunuzi kwa kulipia gharama zote kwa njia ya mtandao.

Huduma hiyo itawahusu wateja wa Tigo ambao simu zao zimesajiliwa katika huduma ya Tigopesa, jambo ambalo litawarahisishia kuepuka kebeba fedha nyingi mkononi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja Bidhaa wa Tigo, William Mpinga, alisema huduma hiyo imezinduliwa leo, kwa lengo la kurahisishia wateja wake kutembea na fedha nyingi kwa ajili ya manunuzi.

Alisema huduma hiyo sasa imesambaa Tanzania nzima kwa mawakala wapatao 50,000, ambao wanauza bidhaa mbalimbali za kijamii.

"Tumeanza tu na hawa, lakini mpango wetu ni kutanuka na kuwafikia watu wengi zaidi kwa kuwaongezea mawakala na kufanya biashara bila kutoa kwanza fedha," alisema.

Alisema kwa sasa, mawakala hao ambao ni wafanyabishara wa bidhaa mbalimbali kwa wananchi wataweza pia kurahisisha ununuzi wa bidhaa hizo kwa kuwafikishia wateja walipo.

"Lakini hili ni kwa wafanyabishara wale ambao tayari walikuwa na utaratibu huu, lakini kwa wale wasiokuwanao wateja watalazimika kununua pale pale wakala alipo," aliongeza Mpinga.

No comments:

Post a Comment