Suluhu Hassan akioneshwa aina mbalimbali za Passpoti ambazo zinatumika hapa nchini na Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji Passpoti na Ukazi, Haji Hamza Khamis, wakati wa ziara yake ya kutembelea Taasisi za Muungano, zilizopo Zanzibar leo. (Picha zote na Ali Meja)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano, Samia Suluhu Hassan, akioneshwa vibali vya Ukazi nchini na Mkuu wa Kitengo cha kuzalishia Passpot na Ukazi, Haji Hamza wakati wa ziara yake ya kutembelea taasisi za Muungano ziliopo Zanzibar leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano, Samia Suluhu Hassan, akiuliza
jambo kwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Mwinchumu Hassan Salum, kwenye chumba cha kutunzia kumbukumbu za Nyaraka za kuzaliwa, wakati
wa kuomba passpoti nchini.
Na Ali Issa- Maelezo Zanzibar, 4/4/2013.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Samia Suluhu Hassan, amewataka Maofisa Uhamiaji wanaokusanya Mapato, kuwa waadilifu katika
ukusanyaji wa mapato yatokanayo na huduma wanazozitoa hapa nchini, ili kuweza
kujitatulia changamoto zinazowakabili.
Hayo ameyasema leo, huko katika Ofisi ya Uhamiaji Kilimani mjini Unguja
wakati alipofanya Ziara ya kuitembelea Idara hiyo ikiwa ni mfululizo wa Ziara
zake ya kuzitembelea Taasisi za Muungano zilizopo Zanzibar.
Amesma iwapo Maafisa hao watafanya kazi kwa uadilifu katika kukusanya
Mapato wataweza kuzitatua changamoto zinazo wakabili katika idara yao na kupiga
hatua mbele.
“Uadilifu unahitajika katika makusanyo ya fedha, kwani mnaweza kudai
kupatiwa mengi na ikawezekana lakini kama hakuna makusanyo mazuri itakuwa
viguma kuyapata mnayoyadai”alisema Samia.
Aidha waziri huyo alisema kuwa iwapo uadilifu utaongezwa
matatizo madogo madogo kama vile uchimbaji wa Kisima na Ufungaji wa Lifti
katika Jengo jipya la Uhamiaji ni rahisi Maafisa hao kuufanya wenyewe ndani ya
kipindi kifupi.
Waziri huyo aliwaeleza wafanyakazi hao kulifanyia kazi suala hilo
pamoja na kuwa na mashirikiano katika kazi na maamuzi wanayoyatoa yawe ya
pamoja bila ya kuwa na malumbano.
Awali akimkaribisha Waziri Samia, Kamishna wa uhamiaji Zanzibar
Mwichum Hassan Salum amemueleza waziri kuwa katika kuleta uadilifu wa
ukusanyaji wa mapato Idara ya uhamiaji imeunzisha Kitengo kinachopambana na
rushwa kwenye huduma zao.
Amesema wameweka mfumo malumu katika Afisi zao kwa ajili ya
kupokea kero na maoni ya wananchi kuhusu utendaji wa kazi zao.
Mwichumu alimueleza Waziri kuwa Idara hiyo inakabiliwa changamoto
mbalimbali ikiwa ni pamoja na uhaba wa watumishi 105 ambapo kwa sasa idadi ni
Watumishi 375 ambao ni wa chache kutokana na majukumu kuongezeka.
Katika hatua nyingine Waziri Samia alitembelea idara ya Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa Ofisi ya Zanzíbar na kuwasihi Watendaji wake kufanya
kazi kwa mujibu wa sheria na uzalendo na bila kumpa mtu yetote asiyestahiki
kitambulisho hicho.
No comments:
Post a Comment