TANGAZO


Thursday, April 4, 2013

Kongamano la kujadili rasimu ya sera ya manunuzi lafanyika jijini Dar es Salaam

Kamishna wa Idara ya Sera ya Manunuzi ya Umma kutoka Wizara ya Fedha, Dk. Frederick Mwakibinga (kulia), akiteta jambo na Clemence Tesha, ambaye ni  mjumbe wa Kamati ya Sera ya manunuzi, wakati wa Kongamano la kujadili rasimu ya Sera ya Manunuzi ya Umma, lililofanyika hivi karibuni,  jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja, lilihudhuriwa na wajumbe mbalimbali kutoka Ofisi za Serikali na Taasisi binafsi nchini. 

Emmanuel Maliganya ambaye ni Ofisa Ugavi kutoka Benki Kuu ya Tanzania, akichangia mada kuhusu Utendaji kazi wa Maofisa Ugavi, wakati wa Kongamano la kujadili rasimu ya Sera ya Manunuzi ya Umma, lililofanyika hivi karibuni,  jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja, lilihudhuriwa na wajumbe mbalimbali kutoka Ofisi za Serikali na Taasisi binafsi nchini. 

Juma Fimbo kutoka Umoja wa Wataalamu wa Manunuzi na Ugavi  Tanzania, akielezea jinsi Maofisa Ugavi, wanavyotakiwa kufanya kazi zao kwa kutumia taaluma ya uchumi wakati wa Kongamano la kujadili rasimu ya Sera ya Manunuzi ya Umma, lililofanyika hivi karibuni,  jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja, lilihudhuriwa na wajumbe mbalimbali kutoka Ofisi za Serikali na Taasisi binafsi nchini. 

Mkurugenzi wa Ugavi kutoka Akaunti ya Changamoto za Milenia (Millenium Challange Account), Marieth Ngaida akichangia mada wakati wa Kongamano la kujadili rasimu ya Sera ya Manunuzi ya Umma, lililofanyika hivi karibuni,  jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja, liliandaliwa na Idara ya Sera ya Manunuzi ya Umma.

Profesa Gaspar Munishi kutoka  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala akielezea  kuhusu umuhimu wa kuboresha rasimu ya Sera ya manunuzi  wakati wa kongamano la kujadili rasimu hiyo lililofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa JB jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya umma. Kulia ni Dk. Godfrey Sansa kutoka Chuo hicho.




Kamishna wa  Idara ya Sera ya manunuzi ya umma kutoka Wizara ya Fedha Dk. Frederick Mwakibinga (kushoto) akisalimiana na Prof. Gaspar Munishi kutoka  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya Sera ya manunuzi ya Umma lililofanyika hivi karibuni  katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa JB jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja lilihudhuliwa na wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi.



Baadhi ya wajumbe kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi wakimsikiliza Prof. Gaspar Munishi kutoka  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala (hayupo pichani) wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya Sera ya manunuzi ya Umma lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na  Idara ya Sera ya manunuzi ya umma.

Khamisi Tikka kutoka Mamlaka ya Rufaa za zabuni   akichangia mada  wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya Sera ya manunuzi ya Umma lililofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa JB jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya umma na kuhudhuliwa na wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi. (Picha zote na Anna Nkinda – Maelezo)


No comments:

Post a Comment