TANGAZO


Tuesday, April 2, 2013

Wapinzani wa Azam FC watua jijini wakiwa na matumaini tele


Wachezaji wa Barack Young Controllers ya Liberia, wakiwa na Afisa wa Shirikisho la soka nchini (TFF), Mzee Mshangama baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataiaf wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

Wachezaji wa Barack Young Controllers ya Liberia, wakitoka uwanjani leo asubuhi.

Wachezaji wa Barack Young Controllers ya Liberia, wakipanda basi la Hoteli wanayofikia leo asubuhi mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo.

Kocha na wachezaji wakiwa ndani ya basi tayari kwa safari ya Hotelini leo asubuhi.

Basi lililowabeba wachezaji wa timu hiyo ya Liberia, inayopambana na Azam FC Jumamosi hii, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mtoto wa Rais wa Liberia,  Robert Alvin Sirleaf (kushoto), akiwa na mmoja wa viongozi, ambaye alikuwa kwenye msafara huo.
Hoteli waliofikia wachezaji wa timu hiyo, jijini Dar es Salaam leo.

Wakishuka kwenye basi hilo na kuingia hotelini.
Wakiwa ndani ya Saphirre Court Hotel, jijini Dar es Salaam leo.

TIMU ya Barrack Young Controllers II ya Liberia imetua leo asubuhi huku ikiwa na matumaini kibao ya kuwafunga wapinzani wao Azam FC.

Naye kocha wa timu hiyo, Robert Lartey, amejigamba kuwa uwezo wa kuifunga Azam FC kwenye mchezo wa marudiano wa kombe la Shirikisho utakaochezwa jijini Dar es Salaam jumamosi kwani makosa yaliyoigharimu timu amekwisha yafanyia marekebisho

“Mchezo huu ni muhimu kwa timu yangu na naamini nitashinda”, alisema Lartey.

Pia alijigamba kuwa na kikosi chenye wachezaji wenye vipaji ambao pia wapo timu ya taifa ya Liberia ya Vijana, akina Ezekiel Doe, Benjamin Gbamy na George Dauda.
Wachezaji wa timu hiyo wameonekana kuwa nyuso zao kutokuwa na furaha sijui ni kwa kutafakari kuwa walipoteza mchezo wa awali wakiwa nyumbani na sasa wanacheza ugenini.

Young Controllers imetua leo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 2:30 kabla ya muda wa 3.35 asubuhi ambao ulitarajiwa kwa ndege ya PrecisionAir ikitokea Nairobi, Kenya inapounganisha safari hiyo inayoanzia Monrovia kupitia Accra, Ghana.

Kocha huyo amesema hali ya hewa ya Dar es salaam haijatofautiana sana na hali ya hewa ya Liberia jana amekiri Dar es Salaam kuwa na joto kuzidi Monrovia

Msafara wa timu hiyo umetuwa na watu 37, wachezaji 21 na unaongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu hiyo Robert Alvin Sirleaf ambaye ni mtoto wa Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, Samuel Sumo wakati Meneja wa timu ni Clarence Murvee. Daktari wa timu ni Samuel Massaquoi.

Wachezaji waliomo kwenye kikosi hicho ni Abraham Andrew, Alfred Hargraves, Alpha Jalloh, Benjamin Gbamy, Cammue Tumamie, Erastu Wee, Ezekiel Doe, George Dauda, Hilton Varney, Ishmail Paasewe, Joekie Solo, Joseph Broh, Junior Barshall, Karleo Anderson, Mark Paye, Prince Jetoh, Prince Kennedy, Randy Dukuly, Raymond Blamonh na Winston Sayou.

No comments:

Post a Comment