Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali
Mohamed Shein, akipata maelezo
kutoka kwa Mwenyekiti wa
Taasisi ya Muzdalifa, Sheikh Abdalla Hadhal, alipokuwa akiangalia
maonesho ya picha mbalimbali, wakati wa maadhimisho ya siku ya
mtoto
Yatima katika Ukumbi wa Salama Bwawani. Maadhimisho
hayo, yamefanywa leo na Shirika la I.H.H la nchini Uturuki kwa
ushirikiano na Jumuiya ya
Muzidalifa ya Zanzibar, inayoshuhulika
na Yatima. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali
Mohamed Shein, akipokea
zawadi kutoka kwa mtoto Hinaina Said
Khalfan, wakati wa sherehe za Siku ya Mtoto yatima zilizofanyika
ukumbi wa Salama Bwawani Hotel leo, Mjini Zanzibar. Hafla hiyo
imeandaliwa na shirika la misaada la I.H.H la Uturuki, kwa
Ushirikiano na Jumuiya ya Muzdalifa ya Zanzibar.
Watoto Yatima waliohudhuria
katika sherehe za maadhimisho ya
siku ya Mtoto
Yatima, wakiwa katika Ukumbi wa Salama Bwawani,
Mjini Zanzibar leo, katika sherehe zilizoandaliwa kwa ushirikiano
na Jumuiya ya Muzdalifa na shirika la
misaada la I.H.H la nchini
Uturuki leo na kuhudhuriwa na wananchi na viongozi mbalimbali.
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali
Mohamed Shein, akipokea
risala kutoka kwa Nasra Suleiman
Abdalla, wakati wa sherehe za
maadhimisho ya Siku ya Mtoto
yatima zilizofanyika leo, katika
ukumbi wa Salama Bwawani, mjini
Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali
Mohamed Shein, akitoa
hutuba yake wakati wa Sherehe ya
maadhimisho ya Siku ya Mtoto Yatima katika ukumbi wa Salama
Bwawani Hoteli, mjini Zanzibar
leo. Maadhimisho hayo,
yamesimamiwa na Jumuiya ya Muzidalifa na Shikika la
misaada la
I.H.H la nchini Uturuki. Kushoto ni Makamo wa Kwanza wa Rais
wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif, Balozi wa Uturuki, nchini Ali
Daudi Gul na Kulia ni Waziri wa
Katiba na Sheria, Abubakar
Khamis Bakary.
No comments:
Post a Comment