TANGAZO


Tuesday, April 2, 2013

Wafungwa 6 wa kisiasa waachiliwa Sudan


Serikali inasema kuachiliwa kwa wafungwa kutaboresha mazingira ya mazungumzo
Wafungwa sita wa kisiasa wameachiliwa nchini Sudan, siku moja baada ya Rais Omar al-Bashir kuamuru kuachiliwa kwa wafungwa wote wa kisiasa.
Jamaa za wafungwa hao waliwakumbatia kwa furaha walipokuwa wanaondoka jela mjini Khartoum.
Wafungwa hao ni pamoja na Abdul Aziz Khalid, aliyekamatwa mwezi Januari baada ya kuunga mkono hatua ya kupindua serikali.
Mnamo Jumatatu, bwana Bashir alisema kuwa alitaka mazungumzo na vyama vya kisiasa ili kusuluhisha tofauti zilizopo.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanamshutumu Bashir aliyechukua mamlaka baada ya mapinduzi ya kijeshi kwa kutawala moja ya serikali zenye kukandamiza watu sana barani Afrika.

Mabadiliko ya utawala

Bwana Khalid alihudhuria mkutano katika nchi jirani ya Uganda mnamo mwezi Januari, wa vyama vya upinzani vya Sudan na makundi ya waasi ambako mwafaka uliafikiwa ukitaka kupinduliwa kwa serikali kwa njia ya amani na kwa kutumia vurugu.
Baada ya kurejea Sudan, alikamatwa akiwa na wenzake watano wa upinzani ingawa kwa sasa wameachiliwa.
Mkutano wa upinzani nchini Uganda ulichochea mgogoro wa kidiplomasia kati ya serikali ya Sudan na Uganda
Sudan ilituhumu Uganda kwa kuidhinisha mageuzi ya utawala mjini Khartoum.
Uganda ilikanusha madai hayo na kusema kuwa nchi hiyo ni huru ambako watu wanaweza kukutana na kuzungumzia mambo yao.
Mwezi jana Bwana Bashir alisema kuwa ataweza kuondoka mamlakani kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 kwa sababu nchi yake inahitaji sasa kuongozwa na vijana.
Bashir anatakikana na mahakama ya kimataifa ya ICC, kwa makosa ya jinai kuhusiana na vita katika jimbo la
Darfur.

No comments:

Post a Comment