Rais wa Afrika Kusini jacob Zuma anahudhuria misa ya wafu mjini Pretoria kwa ajili ya wanajeshi kumi na watatu wa nchi hiyo waliuuwawa katika mapinduzi ya serikali hivi majuuzi katika Jamhuri ya Afrika ya kati.
Walifariki katika makabiliano na waasi karibu na mji mkuu Bangui.
Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kimepuuza madai kuwa wanajeshi hao walikuwa wakimlinda rais Francois Bozize, ili kupata kandarasi za madini kwa ajili ya viongozi wakuu wa ANC.
Upinzani unataka uchunguzi rasmi wa madai hayo.
Zuma alisema kuwa wanajeshi hao walifariki wakiwa wanalinda amani na uthabiti wa bara la Afrika zaidi ya wiki moja iliyopita.
Wakati huohuo, Chama tawala cha ANC, kimekanusha madai ya uhusiano wa kibiashara na Jamuhuri ya Afrika ya Kati uliosababisha vifo vya wanajeshi wake 13.
Wanajeshi hao waliuawa nchini humo mwezi jana wakati waasi walipouteka mji mkuu katika mapinduzi ya kijeshi yaliyomng'oa mamlakani rais Francois Bozize.
Duru zinasema kuwa majeshi ya Afrika Kusini yalikuwa yanalinda ikulu ya Rais huku nchi ikipewa mikataba ya kifahari ya uchimbaji madini.
Serikali ya Afrika Kusini inasema kuwa ilikuwa inatoa mafunzo kwa vikosi vya nchi hiyo pamoja na kutoa usalama.
Kulingana na waziri wa ulinzi wa Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula, takriban wanajeshi 300, walikuwa katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, na walizidiwa nguvu wakati waasi walipouteka mji mkuu kati ya tarehe 23-24.
Wanajeshi 13 waliuawa na wengine 27 walijeruhiwa.
Jarida la Afrika Kusini 'Mail and Guardian' liliripoti kuhusu uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili na kusababisha chama tawala kutishia jarida hilo kuwa litaichukulia hatua za kisheria.
Kilituhumu gazeti hilo, kwa kile ilichosema ni kukojolea makaburi ya wanajeshi walioweka maisha yao hatarini wakihudumia nchi na bara.
"chama cha ANC kinakanusha vikali madai ya jarida la Mail and Guardian kuwa wanajeshi wa Afrika Kusini, walitumwa katika Jamhurui ya Afrika ya Kati kulinda maslahi ya kibiashara ya chama cha ANC.''
Kiliongeza kuwa ANC kama chama hakina maslahi yoyote ya kibiashara nchini humo.
Wakati huohuo, chama cha upinzani Democratic Alliance, kimesema kuwa kitawasilisha hoja bungeni kutaka wanajeshi wa Afrika Kusini kuondolewa nchini humo.
Kiongozi wa chama hicho Bi Helen Zille, alisema kuwa inaonekana kama wanajeshi wa Afrika Kusini walikuwa nchini humo kulinda utawala.
No comments:
Post a Comment