Pages

Friday, April 19, 2013

Ujumbe wa Shirikisho la Fasihi na Sanaa la China watembelea Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo jijini Dar

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Seth Kamuhanda (katikati), akizungumza na ujumbe kutoka Shirikisho la Fasihi na Sanaa nchini China, Dar es Salaam leo, ukiongozwa na Yang Chengzhi (kushoto), waliokuja nchini kwa ajili ya kutembelea kituo cha Tingatinga pamoja na Baraza la sanaa la Taifa (BASATA), kama sehemu ya kujifunza utajiri wa sanaa. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni, Profesa Hermas Mwansoko. (Picha na Beatrice Mlyansi-MAELEZO)

Wajumbe wa Shirikisho la Fasihi na Sanaa kutoka China, wakimsikiliza Katibu Mkuu  Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Seth Kamuhanda (hayupo pichani), wakati alipokuwa akilishukuru shirikisho hilo kwa kukipatia vifaa Chuo cha Sanaa Bagamoyo, Dar es Salaam leo. Kulia ni Bi. Yang Chengzhi, aliyekuwa akiuongoza Ujumbe huo. 


Kiongozi wa Ujumbe wa Shirikisho la Fasihi na Sanaa kutoka China, Bi. Yang Chengzhi akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu ziara yao nchini pamoja na kazi zinazofanywa na shirikisho hilo katika kukuza fasihi na sanaa nchini China na dunia.

No comments:

Post a Comment