Wajumbe wa Shirikisho la Fasihi na Sanaa kutoka China, wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Seth Kamuhanda (hayupo pichani), wakati alipokuwa akilishukuru shirikisho hilo kwa kukipatia vifaa Chuo cha Sanaa Bagamoyo, Dar es Salaam leo. Kulia ni Bi. Yang Chengzhi, aliyekuwa akiuongoza Ujumbe huo.
Kiongozi wa Ujumbe wa Shirikisho la Fasihi na Sanaa kutoka China, Bi. Yang Chengzhi akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu ziara yao nchini pamoja na kazi zinazofanywa na shirikisho hilo katika kukuza fasihi na sanaa nchini China na dunia.




No comments:
Post a Comment