Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sethi Kamuhanda, akizungumza wakati akifungua mafunzo elekezi ya siku mbili kwa watumishi wapya wa wizara hiyo, leo katika ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2012/13, imeajiri watumishi wapya 30.
Waajiriwa wapya kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Wakurugenzi wa Idara na Baadhi ya wafanyakazi wa wizara hiyo, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa mafunzo elekezi leo, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Wa tatu kushoto, mstari wa mbele ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Sethi Kamuhanda.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Barnabas, Ndunguru (kulia), akimweleza jambo Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Sethi Kamuhanda mara baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa mafunzo elekezi kwa watumishi wapya leo katika ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Baadhi wa waajiriwa wapya wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakimsikiliza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Sethi Kamuhanda (hayupo pichani), wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi yaliyofanyika leo, ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sethi Kamuhanda, akiongea jambo leo na watumishi wapya wa wizara hiyo, wakati wa mafunzo elekezi yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2012/13, imeajiri watumishi wapya 30, ambao wengi wao ni vijana.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Sethi Kamuhanda (hayupo pichani), wakati akifungua mafunzo elekezi ya siku mbili kwa watumishi wapya wa wizara hiyo leo, ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene.
Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Herman Mwasoko, akiongea jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi ya siku mbili kwa watumishi wapya wa wizara hiyo, yaliyofanyika leo, katika ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Enely Mwakyoma na kushoto ni Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo.
No comments:
Post a Comment