TANGAZO


Tuesday, April 23, 2013

Dk. Shein afanya ziara ya kichama Mjini Unguja

Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Mjini Unguja pamoja na viongozi mbalimbali walioalikwa katika mkutano huo, uliofanyika jana katika ukumbi wa Ofisi ya Mkoa Amani, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiri wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, alipokuwa akizungumza nao jana alipofanya ziara ya kuimarisha chama chake katika Mkoa huo. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, kabla ya kuzungumza na wajumbe wa Kamati ya Siasa, Mkoa wa Mjini na Wilaya za Amani na Mjini pamoja na viongozi mbalimbali, walioalikwa katika mkutano huo, uliofanyika jana ukumbi wa Ofisi ya Mkoa, Amani mjini Unguja, alipofanya ziara ya kuimarisha Chama chake hicho, mkoani humo. 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Siasa, Mkoa wa Mjini na Wilaya za Amani na Mjini Unguja pamoja na viongozi mbalimbali walioalikwa katika mkutano huo, uliofanyika jana, ukumbi wa Ofisi ya Mkoa Amani, alipofanya ziara ya kuimarisha chama chake mkoani humo.


Meneja wa Benki ya Ushirika wa wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Kikwajuni Saccos Benk, Abdulrahim Abdulrahman Khatib (kulia), akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, mara baada ya kuifungua Benki hiyo, jana alipokuwa katika ziara ya kuimarisha chama chake Mkoa wa Mjini Unguja. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Tatu Tawakal Khamis.

Baadhi ya wanachama wa CCM wa Jumuiya ya Kikwajuni Saccos Bank na wananchi, walioalikwa wakiwa katika sherehe za uzinduzi wa Benki ya Saccos hiyo,  zilizofanyika katika viwanja vya Kisiwandui, Mjini Unguja, ambapo Mgeni rasmi katika sherehe hizo alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, akimakabidhi cheki ya sh. laki tatu, Fatma Makame Issa, akiwa miongoni mwa wanachama wa Kikwajuni Saccos Benki, waliobahatika kupatiwa mikopo baada ya uzinduzi rasmi wa saccos hiyo jana.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, akizungumza na wanachama wa CCM wa Kikwajuni 
Saccos Bank, pamoja na waalikwa katika sherehe za uzinduzi wa
Benki hiyo jana huko Kisiwandui, Mjini Unguja, akiwa  katika 
ziara ya  kuimarisha chama chake, Mkoa wa Mjini. Kulia ni  Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mjini, Borafya Silima Juma na kushoto ni Mwenyekiti wa Kikwajuni Saccos Bank, Tatu Tawakal Khamis.

Vijana wa CCM Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam waliowaunga mkono, wenzao wa Wilaya ya Mjini, wakitumbuiza wakati wa mkutano wa chama hicho, uliohutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Uwanja wa Kisonge, mjini Unguja jana, alipokuwa katika ziara ya kuimarisha chama chake cha Mapinduzi kwa wilaya hiyo.



Vijana wa kikundi cha UB 40 cha Magomeni, Jimbo la Mpendae, wakitoa burudani wakati wa mkutano wa CCM, uliohutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Uwanja wa Kisonge jana, alipokuwa katika ziara ya kuimarisha chama chake, Wilaya ya Mjini Unguja.

No comments:

Post a Comment