TANGAZO


Friday, April 26, 2013

Rais Kikwete awaongoza wananchi katika maadhimisho ya miaka 49 ya Muungano

Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungi wanchi, wakati alipokuwa akiiingia Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam tayari kuwaongoza maelfu ya watu waliohudhuria kilele cha sherehe za Miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika leo.

Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungi wanchi, wakati alipokuwa akiiingia Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam tayari kuwaongoza maelfu ya watu waliohudhuria kilele cha sherehe za Miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika leo.

Amiri Jeshi mkuu, Rais Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa gwaride rasmi lilioandaliwa katika kuadhimisha miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika sherehe zilizofanyika leo asubuhi katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Amiri Jeshi mkuu, Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa gwaride rasmi lilioandaliwa katika kuadhimisha miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika sherehe zilizofanyika leo asubuhi katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wananchi waliofurika wakiwa katika uwanja wa Uhuru jiji Dar es Salaam kuhudhuria maadhimisho ya Sherehe za miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange wakati wa kilele cha Sherehe za miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo asubuhi. (Picha zote na Freddy Maro) 
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete akikagua gwaride la heshima wakati wa sherehe za miaka 49 ya Muungano kwenye Uweanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.
Vikosi vya Jeshi la Wananchi na Polisi vikiwa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 49 ya Uhuru, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaa leo.
Vikosi vya Jeshi la Wananchi vikipita kwa ajili ya kutoa heshima zao kwa Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete, Uwanja wa Uhuru jijini leo.
Kikosi cha Jeshi la Wanamaji (Nevy), kikipita mbele ya Rais Jakaya Kikwete Uwanjani hapo leo.

Kiapo cha Utii kwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete.

Vikosi cha Jeshi la Wannchi, vikiwa katika maadhimisho hayo, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam leo. 
Ndege za kivita zikifanya maonesho katika sherehe za maadhimisho ya miaka 49 ya Muungano jijini Dar es salaam leo, zenye rangi ya njano zinazomwaga rangi za bendera za Taifa ni ndege za mafunzo na zingine za kijivu ni za kivita. (Picha na Issa Michuzi)


Na Salum Vuai, Dar es Salaam
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, leo aliwaongoza maelfu ya Watanzania katika sherehe za maadhimisho ya miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Sherehe hizo zilifanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wote wa kitaifa nchini, mawaziri wa Serikali ya Muungano na ile ya Mapinduzi Zanzibar, viongozi wa ngazi zote na watendaji wakuu pamoja na wananchi mbalimbali.
Baadhi ya viongozi hao ni pamoja na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza na wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad na Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, na Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Peter Pinda.
Wengine ni Marais wastaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi na Benjamin William Mkapa, Rais mstaafu wa Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume, Mawaziri Wakuu wastaafu Fredrick, Sumaye, Edward Lowasa na John Malecela, Spika wa Bunge Anne Makinda na Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho na viongozi wengine.
Pamoja na mvua ya wastani iliyokuwa ikinyesha mapema asubuhi, wananchi mbalimbali walijitokeza kwa wingi uwanjani hapo kusherehekea Muungano huo wa kihistoria ulioziunganisha nchi za Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, mwaka 1964.
Shamrashamra mbalimbali zilipamba sherehe hizo, likiwemo gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama, halaiki ya muungano wa wanafunzi kutoka Zanzibar na Bara, ngoma za asili, Sindimba kutoka mkoani Lindi, Gonga-Kusini Pemba na Nyaketari kutoka Tarime, Mara.
Aidha, kikosi cha kwaya cha JKT Msange kutoka mkoa wa Tabora, nacho kilishuka uwanjani kuhitimisha maadhimisho hayo, ambapo kilitia fora kutokana na manjonjo ya kiongozi wake aliyekuwa kivutio kikubwa uwanjani hapo.
Mapema baada ya kuwasili uwanjani hapo, Rais Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi wa maadhimisho hayo, alipigiwa mizinga 21 na kukagua vikosi vya gwaride, kabla kupokea saluti ya utii kwa Rais.
Baada ya hapo, vikosi mbalimbali vya gwaride vilipita mbele ya mgeni rasmi na waalikwa wengine, kwa mwendo wa polepole na ule wa haraka, huku vikishangiriwa kwa nguvu na wananchi waliovutiwa na ukakamavu wa wapiganaji hao.
Kwa upande wao, vijana wa halaiki walinogesha sherehe hizo kwa kuonesha sura nne za maonesho, ambayo ni ulinzi, uchumi, afya na utamaduni, na kumalizia kwa sarakasi iliyowafurahisha wageni na wananchi wote waliohudhuria sherehe hizo.
Miongoni mwa maumbo waliyotengeneza na kufurahisha umma, ni maandishi yaliyosomeka “Miaka 49 ya Muungano”, pamoja na “Tusichanganye Kiswahili na Lugha nyengine”.
Tukio jengine lililosisimua hadhira uwanjani hapo, ni maonesho ya ndege za kivita za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), zilizoruka katika anga ya uwanja huo, huku zikitoa moshi wenye ishara ya bendera ya Taifa.
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliasisiwa Aprili 26, 1964 kutokana na makubaliano ya Rais wa kwanza wa Tanganyika Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyeyere, na aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Abeid Amani Karume.
Sherehe za mwaka huu zinabebwa na kaulimbiu isemayo, “Amani, utulivu na maendeleo ni matokeo ya muungano wetu, tuulinde na kuutunza.

No comments:

Post a Comment