TANGAZO


Monday, April 1, 2013

Rais Kikwete akutana na Naibu Rais wa Kenya, William Ruto, Serengeti, mkoani Mara


Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akisalimiana na Naibu Rais mteule wa Kenya, William Kipchirchir Samoei arap Ruto,  leo April 1, 2013 katika Hoteli ya Kitalii ya Seronera kwenye mbuga ya wanyama ya Serengeti, mkoani Mara. Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka. (Picha zote na Ikulu)


 Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akisalimiana na Mama Rachel Chebet, mke wa  Naibu Rais mteule wa Kenya, William Kipchirchir Samoei arap Ruto, leo April 1, 2013 katika Hoteli ya Kitalii ya Seronera kwenye mbuga ya wanyama ya Serengeti, mkoani Mara. Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akiongea na Naibu Rais mteule wa Kenya, William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika Hoteli ya Kitalii ya Seronera leo April 1, 2013 katika mbuga ya wanyama ya Serengeti, mkoani Mara. Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.



Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akimuongoza kuelekea kwenye chakula cha mchana, Naibu Rais mteule wa Kenya, William Kipchirchir Samoei arap Ruto na mkewe Rachel Chebet katika Hoteli ya Kitalii ya Seronera  leo April 1, 2013, katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.



Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akipozi kwa picha na familia ya Naibu Rais mteule wa Kenya, William Kipchirchir Samoei arap Ruto, leo April 1, 2013 katika Hoteli ya Kitalii ya Seronera kwenye Mbuga ya wanyama ya Serengeti, mkoani Mara. Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013, amekutana na Naibu Rais mteule wa Kenya, William Kipchirchir Samoei arap Ruto,  ambaye alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.

Akiongea na mgeni huyo katika Hoteli ya Seronera iliyoko katika mbuga ya wanyama ya Serengeti, mkoani Mara, Rais Kikwete, amempongeza Ruto na Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta kwa ushindi wao kwenye uchaguzi mkuu nchini Kenya.

Rais pia alimueleza Rutto furaha yake pamoja na kuridhishwa  na jinsi uchaguzi ulivyofanyika kwa amani katika nchi hiyo.

Alielezea matumaini yake ya kuwa urafiki uliopo kati ya Tanzania na Kenya, utadumishwa pamoja na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Rutto, ambaye aliwasili mkoani Mara wiki iliyopita, akiwa na mke wake na watoto, ameondoka leo baada ya chakula cha mchana alichoandaliwa na mwenyeji wake.


No comments:

Post a Comment