Mahakama ya juu zaidi nchini India imekataa ombi la kampuni ya madawa ya Norvatis kulinda dawa yake mpya ya Saratani Glivec kutokana na kuigizwa na makampuni yanayotengeza dawa za bei nafuu nchini humo.
Kampuni hiyo ya Uswizi awali ilinyimwa idhini ya kufanya hivyo na maafisa wakuu nchini humo wakisema kuwa dawa hiyo mpya ina utofauti mdogo sana na dawa asilia.
Kulikuwa na wasiwasi kuwa ikiwa mahakama ingekubali ombi hilo, ingetishia uwezekano wa watu maskini kuweza kupata madawa ya bei nafuu katika nchi maskini ungepungua.
Lakini makampuni katika nchi za Magharibi, yalionya kuwa uamuzi wowote dhidi ya kampuni hiyo ungeweza kuzuia uekezaji katika utafiti wa madawa.
Dawa ya Glivec, ambayo hutumiwa kutibu saratani ya damu na aina nyingine za Saratani, inagharimu dola 2,600 kwa mwezi.
Dawa mbadala au ile iliyoigizwa inauzwa kwa dola 175 nchini India.
''Hatua hii itawasaidia watu wengi kuweza kupata madawa ya bei nafuu katika nchi maskini,'' alisema Anand Grover,wakili aliyewawakilisha shirikisho la msaada kwa wagonjwa wa Saratani nchini India.
Wakili huyo aliongeza kuwa madawa yatakayolindwa na sheria dhidi ya kuigizwa yatakuwa yale yaliyobuniwa wala sio yale yaliyofanyiwa mabadiliko kidogo.
Novartis iliwasilisha ombi la kutaka dawa hiyo kulindwa mwaka 2006, ikisema kuwa sasa imeboreshwa zaidi.
Maafisa pia walikataa ombi la kampuni hiyo miaka mitatu iliyopita
No comments:
Post a Comment