TANGAZO


Friday, April 5, 2013

Mikutano Mikuu ya Mitaa ya Mabaraza ya Katiba yafanyika wilayani Temeke leo

Mkazi wa Mtaa wa Mivinjeni, Kata ya Kurasini, wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam, aliyewania nafasi ya uwakilishi wa Vijana katika Mikutano wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya, Sophia Stephen, akijinadi mbele ya wananchi wa mtaa huo, kabla ya kufanyika kwa Mkutano Mkuu maalum wa mtaa kwa ajili ya kuwachagua wananchi watakaopendezwa kuwa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya katika mtaa huo leo, Ijumaa April 5, 2013.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Shimo la Udongo, Kata ya Kurasini, Wilaya ya Temeke, mkoani Dar es Salaam, Issa Chigona akizungumza na wananchi wa mtaa huo, kabla ya kufanyika kwa Mkutano Mkuu maalum wa mtaa huo, kwa ajili ya kuwachagua wananchi watakaopendekezwa kuwa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya leo, Ijumaa, April 5, 2013.

Wakazi wa mtaa wa Buza, Kata ya Buza wilayani Temeke, mkoani Dar es Salaam, wakifuatilia kwa makini kikao cha mkutano mkuu maalum wa mtaa huo, kwa ajili ya kuchagua wananchi watakaopendekezwa kuwa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya katika mtaa huo leo, Ijumaa, April 5, 2013


Wagombea wa nafasi za uwakilishi wa wanawake katika kikao cha Mkutano Mkuu maalum wa Mtaa wa Buza, Kata ya Buza wilayani Temeke, mkoani Dar es Salaam, wakionyesha nambari zilizotumika kuwachagua wananchi waliopendekezwa kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya. Kikao hicho, kimefanyika katika shule ya Msingi Buza leo, Ijumaa April 5, 2013.



Wananchi wa mtaa wa Buza, Kata ya Buza, Wilaya ya Temeke, mkoani Dar es Salaam, wakipiga kura za kuwachagua wananchi watakaopendekezwa kuwa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya hiyo, wakati wa mkutano mkuu maalum wa mtaa huo, uliofanyika katika Shule ya Msingi Buza jijini leo, Ijumaa April 5, 2013. (Picha zote na Tume ya Katiba)

No comments:

Post a Comment