Majaji wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu Jaji Mstaafu,
Justice Ernest Mwipopo, wakilishusha katika gari kwa ajili ya
kuanza shughuli za kuaga katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na OMR)
Majaji wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu Jaji Mstaafu,
Justice Ernest Mwipopo, wakilishusha katika gari kwa ajili ya
kuanza shughuli za kuaga katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam leo.
Mmoja wa Majaji, akibeba picha ya marehemu Justice Mwipopo,
wakati majaji hao, wapokuwa wakilishusha jeneza, lenye mwili wa
marehemu huyo, kwa ajili ya kuanza shughuli za kuuaga, Viwanja
vya Karimjee leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Jaji Mkuu Kiongozi, Fakhi Jundu (kushoto) na Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othmani, wakati akiwasili kwenye Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam leo, kushiriki kwenye shughuli za kuuaga mwili wa marehemu Jaji Mstaafu, Justice Ernest Mwipopo, aliyefariki kwa ajali ya gari, April 3, huko maeneo ya Morogoro.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu Jaji mstaafu, Justice Ernest Mwipopo, aliyefariki kwa ajali ya gari April 3, huko maeneo ya Morogoro. Shughuli hizo za kuaga mwili huo, zimefanyika leo, April 5, 2013, Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, ambapo baada ya shughuli hizo, mwili huo, ulisafirishwa kuelekea mkoani Iringa kwa maziko kesho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanaznia, Dk.
Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji ndugu wa marehemu baada ya
kutoa heshima za mwisho, wakati wa shughuli za kuuaga mwili wa
marehemu Jaji Mstaafu, Justice Ernest Mwipopo, aliyefariki kwa
ajali ya gari April 3, huko maeneo ya Morogoro. Shughuli hizo za
kuuaga mwili huo, zimefanyika leo April 5, 2013, Viwanja
vya Karimjee jijini Dar es Salaam, ambapo baada ya shughuli hizo
mwili ulisafirishwa kuelekea mkoani Iringa kwa maziko kesho.
Mmoja wa wanafamilia akibugujikwa na machozi wakati wa
shughuli hiyo ya kuuaga mwili, Viwanja vya Karimjee jijini Dar es
Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanaznia, Dk.
Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Spika wa
Bunge, Anne Makinda, Jaji Mkuu Kiongozi, Fakhi Jundu na Jaji
Mkuu, Mohamed Chande Othmani, wakiwa katika shughuli hiyo,
ya kuuaga mwili huo.
No comments:
Post a Comment