TANGAZO


Saturday, April 27, 2013

Makamu wa Rais, Dk. Bilal ashiriki harambe ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Tanzania Methodist, Msasani na uzinduzi wa CD ya Kwaya ya watoto

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Kanisa la Tanzania Methodist la Msasani, Joseph Mayala leo, Aprili 27, 2013 wakati wa hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha Kanisa hilo, iliyofanyika sambamba na ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya Shirika la Compassion International Tanzania kwa kuingia Ushirika wenza na Makanisa ya Mkoa wa Dar es Salaam na kuzindua CD ya Kwaya ya Watoto wanaofadhiliwa na shirika hilo. Kulia ni Askofu wa Kanisa hilo, Dk. Mathew Byamungu. (Picha zote na OMR)

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya maua kutoka kwa watoto wa Kituo cha Kanisa la Tanzania Methodist la Msasani, wakati alipowasili katika kituo hicho leo, Aprili 27, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha Kanisa hilo, iliyofanyika sambamba na ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya Shirika la Compassion International Tanzania kwa kuingia Ushirika wenza na Makanisa ya Mkoa wa Dar es Salaam na kuzindua CD ya Kwaya ya Watoto wanaofadhiliwa na Shirika hilo.

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia waumini wa dini ya Kikristo wa Kituo cha Kanisa la Tanzania Methodist la Msasani, wakati alipowasili katika kituo hicho leo, Aprili 27, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha Kanisa hilo iliyofanyika sambamba na ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya Shirika la Compassion International Tanzania kwa kuingia Ushirika wenza na Makanisa ya Mkoa wa Dar es Salaam na kuzindua CD ya Kwaya ya Watoto wanaofadhiliwa na Shirika hilo.

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili katika Kituo cha Kanisa la Tanzania Methodist la Msasani leo, Aprili 27, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha Kanisa hilo, iliyofanyika sambamba na ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya Shirika la Compassion International Tanzania kwa kuingia Ushirika wenza na Makanisa ya Mkoa wa Dar es Salaam na kuzindua CD ya Kwaya ya Watoto wanaofadhiliwa na Shirika hilo.

Baadhi ya waumini waliohudhuria harambee hiyo, wakiwa katika ibada maalum ya kumshukuru Mungu.

Wanakwaya inayofadhiliwa na Shirika la Compassion International Tanzania, wakitoa burudani ya kuimba moja ya wimbo wao, ulio katika Albam yao, iliyozinduliwa katika hafla hiyo.

Wanakwaya inayofadhiliwa na Shirika la Compassion International Tanzania, wakitoa burudani ya moja ya wimbo wao, ulio katika Albam yao katika hafla hiyo.

Askofu wa Kanisa la Tanzania Methodist la Msasani, Dk. Mathew Byamungu, akitoa neno la shukrani baada ya hafla hiyo.

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya wachungaji na watumishi wa Kanisa hilo.

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na watoto wanaounda kundi la Kwaya ya watoto, inayofadhiliwa na Shirika hilo.


Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na Watoto.

No comments:

Post a Comment