TANGAZO


Saturday, April 27, 2013

Warsha ya kuhamasisha vijana wa Vyuo Vikuu kujiandaa katika ajira yafanyika Chuo Kikuu (UDSM) jijini

Rais wa Chama cha Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (AIESEC), Frank Mushi, akiongea katika warsha ya 14,  inayohamasisha vijana kujianda katika ajira pindi wanapomaliza masomo ya vyuo vikuu. Warsha hiyo, ilidhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) leo.

Ofisa raslimali watu wa Vodacom Tanzania, Stephen Kisanko, akitoa mada kwa wanafunzi  wa Vyuo Vikuu, juu ya maandalizi na umuhimu wa vijana kujiandaa katika kuingia kwenye ajira pindi wamalizapo masomo yao, wakati wa warsha ya 14 inayohamasisha vijana kujianda katika ajira, warsha iliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) leo.

Ofisa raslimali watu wa Vodacom Tanzania, Stephen Kisanko, akitoa mada kwa wanafunzi  wa Vyuo Vikuu, juu ya maandalizi na umuhimu wa vijana kujiandaa katika kuingia kwenye ajira pindi wamalizapo masomo yao, wakati wa warsha ya 14 inayohamasisha vijana kujianda katika ajira, iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) leo.


Ofisa raslimali watu wa Vodacom Tanzania, Stephen Kisanko, akisikiliza maswali mbalimbali kutoka kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu 13, waliohudhuria warsha ya maandalizi na umuhimu wa vijana kujiandaa katika kuingia kwenye ajira pindi wamalizapo masomo yao. Warsha hiyo ya 14 imedhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa Nkuruma, Chuo kikuu cha Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment