TANGAZO


Monday, April 22, 2013

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais Dk. Shein, aanza ziara ya kichama Mjini Unguja, awataka wananchi na wanachama kuimarisha amani

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar,  akisalimiana na viongozi wa Tawi la CCM,  Vikokotoni, alipofika kuweka jiwe la msingi, akiwa katika ziara ya kuimarisha chama chake, Mkoa wa Mjini leo. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)

Wanachama wa CCM, Tawi la Vikokotoni, walipokuwa wakimshangilia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, alipokuwa akiweka jiwe la msingi la tawi hilo leo, akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Unguja leo. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, akifungua pazia kuweka jiwe la msingi  la Tawi la Chama hicho, Vikokotoni, Mjini Unguja leo, akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama, wilayani humo. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, akizungumza na wananchi pamoja na wanachama wa CCM, tawi la Vikokotoni, Mjini Unguja leo, alipokuwa katika ziara ya kuimarisha Chama, Wilaya ya Mjini leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mjini, Borafya Silima. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,  akizungumza na wananchi pamoja na wanachama wa CCM, Tawi la Vikokotoni, Mjini Unguja leo, alipokuwa katika ziara ya kuimarisha Chama, Wilaya ya Mjini leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, akisalimiana na Viongozi wa CCM, alipowasili kuitembelea Maskani Kaka ya Kisonge, iliyomwa moto na Watu wasiojulikanwa akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mjini leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ,akipata maelezo kutoka kwa  Katibu wa Kamati ya Ujenzi Omar Saidi, wakati alipotembelea Maskani Kaka ya Kisonge, iliyomwa moto na Watu wasiojulikanwa akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mjini leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,(katikati) akifuatana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai,(kulia) pamoja na viongozi wengine baada ya kuitembelea Maskani Kaka ya Kisonge,iliyomwa moto na Watu wasiojulikanwa akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mjini leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Borafya Silima Juma,alipowasili Ofisi ya Mkoa Amani,alipoanza ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi katika Mkoa huo leo,(katikati) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akivalishwa Skafu na Kijana Chipukizi wa CCM Pili Hassan,miaka 10 Mkaazi wa Meli Nne, alipowasili katika Ofisi ya CCM Mkoa Amani,alipoanza ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi katika Mkoa huo leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akisalimiana na Viongozi wa CCM alipowasili katika Ofisi ya CCM Mkoa Amani, alipoanza ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi katika Mkoa huo leo, 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akisalimiana na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM alipowasili katika Ofisi ya CCM Mkoa Amani,alipoanza ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi katika Mkoa huo leo.



Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar  
MAKAMO Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza kuimarishwa kwa amani, umoja na mshikamano na kueleza kuwa vurugu sio utamaduni wa wananchi wa Zanzibar.

Dk. Shein aliyasema hayo leo kwa nyakati tofauti katika ziara yake ya  Chama katika Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Chama Mjini.

Makamo Mwenyekiti huyo alieleza kuwa amani na utulivu ndio msingi wa mafanikio na ndio maana chama hicho cha CCM kimekuwa kikisimamia na kudumisha jambo hilo kwa kutambua umuhimu wake.

Alisisitiza kuwa tayari Zanzibar imeshajijengea sifa kubwa Kimataifa kutokana na mafanikio makubwa yaliopatikana katika kuimarisha na kuiendeleza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yenye mfumo wa Umoja wa Kitaifa, hivyo kujitokeza kwa watu wachache kutaka kuvuruga amani serikali haitowafumbia macho.

Alieleza kuwa wananchi wote wa Zanzibar wana haki sawa na ndio maana Serikali anayoiongoza chini ya chama cha Mapinduzi haimbagui mtu kwa jinsia, rangi, dini ama ukabila.

Alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyo na mfumo wa  Serikali ya Umoja wa Kitaifa haitomvumilia mtu yeyote atakaevuruga amani na utulivu uliopo nchini.

Katika hotuba zake, Dk. Shein aliwasisitiza wanaCCM kuendeleza utamaduni wao wa kuimarisha amani na utulivu na kuzidisha mashirikiano kwani ndio ngao ya ushindi wa chama hicho.

Aidha, Dk. Shein alisisitiza kuwa Serikali anayoiongoza itaendelea kuyalinda na kuyadumisha Mapinduzi ya Januari 12, 1964 sanjari na kuulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Mapema Dk. Shein alipokea taarifa ya kazi za Chama ya Mkoa wa Mjini na baada ya hapo alifika Kisiwandui na kwa ajili ya kuzindua rasmi Benki ya SACCOS ya Umoja wa Wajasiriamali wadogowadogo na kueleza kuwa hatua hiyo ni miongoni mwa utekelezaji wa  Ilani ya CCM.

Baada ya hapo Makamu huyo wa CCM Zanzibar alikwenda Vikokotoni kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi jengo jipya la ghorofa mbili la Tawi la CCM Vikokotoni lililojengwa kwa ubia kati ya Tawi na mfanyabiashara.

Dk. Shein alimalizia ziara yake kwa Wilaya ya Mjini, Dk. Shein alitembelea maskani ya Kisonge iliyopo Michenzani na kuangalia uharibifu uliotokea baada ya kuchomwa moto kwa maskani hiyo wakati wa vurugu zilizotokezea hivi karibuni na kusababisha hasara kubwa ya zaidi ya milioni 50.

Sambamba na hayo, Dk. Shein aliwakabidhi kadi wanachama wapya  270 kutoka Jumuiya zote za CCM zikiwemo wazazi, Umoja wa Wanawake na UVCCM na baadae alisalimiana na wana CCM na kuwataka wanaCCM kuwafundisha siasa vyama vyengine ambavyo vimeonesha kutoelewa maana na umuhimu wa amani na utulivu.

Katika ziara hiyo burudani mbali mbali zilitumbuiza zikiwemo ngoma, nyimbo, mashairi, tenzi pamoja na burudani maalum iliyotolewa na   vijana wa CCM kutoka Ilala, Dar-es-Salaam waliyoitoa katika viwanja vya Kisonge mjini Zanzibar. Ziara hiyo itaendelea kesho katika Wilaya ya Amani.

No comments:

Post a Comment