TANGAZO


Monday, April 22, 2013

Rais Kikwete aufungua Mkutano wa 368 wa Baraza la Amani na Usalama la AU jijini Dar es Salaam, utakao jadili amani ya Madagasca


Rais Jakaya Kikwete, akizungumza wakati alipokuwa akiufungua mkutano wa 368 wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa nchi za Afrika (AU), jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mjumbe wa baraza hilo, Ramtane Lamamra. (Picha zote na Kassim Mbarouk)


Rais Jakaya Kikwete, akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa 368 wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa nchi za Afrika (AU), jijini leo. Kulia ni Mjumbe wa baraza hilo, Ramtane Lamamra.


Wajumbe wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa nchi za Afrika (AU), wakimsikiliza Rais Kikwete, wakati alipokuwa akiufungua mkutano wa 368 wa baraza hilo, ambao unafanyika nchini kwa mara ya kwanza.


Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa nchi za Afrika (AU), wakiwa katika mkutano wa 368 wa baraza hilo, ambao unafanyika nchini kwa mara yake kwanza na kufunguliwa na Rais Jakaya Kikwete jijini leo.


Baadhi ya Mabalozi wa nchi mbalimbali za Afrika, wakiwa kwenye mkutano huo, wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa nchi za Afrika (AU), wakimsikiliza Rais Kikwete, wakati alipokuwa akiufungua mkutano wa 368 wa baraza, ambao unafanyika nchini kwa mara yake kwanza.

Rais Jakaya Kikwete, akisisitiza jambo, wakati alipokuwa akiufungua mkutano wa 368 wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa nchi za Afrika (AU), Dar es Salaam leo. Kulia ni Mjumbe wa baraza hilo, Ramtane Lamamra.



Rais Jakaya Kikwete, akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Baraza hilo, wakati alipokuwa akiufungua mkutano wao wa  368, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mjumbe wa baraza hilo, Ramtane Lamamra.



Rais Jakaya Kikwete, akibadilishana mawazo na Mjumbe wa baraza hilo, Ramtane Lamamra, mara baada ya kuufungua mkutano wa baraza hilo leo asubuhi, jijini Dar es Salaam.

Mjumbe wa baraza hilo, Ramtane Lamamra, akimweleza jambo Rais Jakaya Kikwete, mara baada rais kuufungua mkutano huo. Kushoto ni msuluhishi wa mzozo wa nchi ya Madagasca, Rais mstaafu wa Msumbiji, Joachim Chisano na wa pili kushoto ni Mwenyekiti mpya wa baraza hilo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Benard Membe.


Rais Jakaya Kikwete (katikati waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU), mara baada ya kuufungua mkutano wa 368 wa kujadili amani ya Madagasca, Dar es Salaam leo. Wa pili kushoto ni msuluhishi wa mzozo wa Madagasca, Rais mstaafu wa Msumbiji, Joachim Chisano.

Rais Jakaya Kikwete, akibadilishana mawazo na msuluhishi wa mzozo wa nchi ya Madagasca, Rais mstaafu wa Msumbiji, Joachim Chisano kwenye mkutano wa 368 wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU), jijini Dar es Salaam leo.

Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Mussa Azzan Zungu, baada ya kuufungua mkutano huo, unaojadili amani ya Madagasca jijini leo. Katikati ni Mwenyekuti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, Anna Abdallah.

Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kuufungua mkutano wa 368 wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa nchi za Afrika (AU), jijini Dar es Salaam leo.

Rais Jakaya Kikwete, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari,  wakati alipokuwa akizungumza nao, mara baada ya kuufungua mkutano wa 368 wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa nchi za Afrika (AU), jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Mwenyekiti mpya wa baraza hilo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Benard Membe.

No comments:

Post a Comment