Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali
Mohamed Shein,akipata malezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Maji ZAWA,Dk.Mustafa Ali Garu, alipotembelea shughuli za ujenzi
wa Tangi la Maji safi, katika mradi wa maji vijijini uliofadhiliwa
na Benki ya maendeleo ya Afrika(ADB), huko Gombani, akiwa katika
ziara ya Mkoa wa KusiniI Pemba leo.(Picha zote na Ramadhan Othman,Ikulu)
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Maji ZAWA, Dk. Mustafa Ali Garu (kushoto), akitoa
maelezo ya michoro ya kazi ujenzi wa Tangi la Maji
safi, katika mradi wa maji vijijini uliofadhiliwa na Benki ya maendeleo
ya Afrika (ADB)kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein(kushoto), alipotembelea shughuli hizo
leo, huko Gombani, akiwa katika ziara ya Mkoa wa Kusini Pemba leo.
Mkurugenzi
Mkuu shirika la Utangazaji ZBC Hassan Abdalla Mitawi, akitoa
maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
Dk. Ali Mohamed Shein(kushoto), alipotembelea shughuli za Digital
katika kituo cha Tv Mkanjuni Pemba, akiwa katika ziara ya Mkoa wa KusiniI Pemba leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Agape Association Ltd, Dk. Vernon Fernanders.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Agape Association Ltd, Dk.Vernon Fernanders, akitoa maelezo kwa
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein pamoja na
ujumbe wake, kuhusu kutoka Analogi kwenda Dijital katika kituo cha Tv Mkanjuni Pemba leo, wakati wa Ziara ya
Rais kuangalia shuhuli mbali mbali za maendeleo katika Wilaya ya Chake chake
Mkoa wa Kusini Pemba.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Agape Association Ltd, Dk.Vernon Fernanders, akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, namna ya king'amuzi kinavyoweza kufanya kazi wakati wa kuanza kutumia Digital alipotembelea kituo cha Tv Mkanjuni Pemba leo, wakati wa Ziara ya Rais kuangalia shuhuli mbalimbali za maendeleo katika Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali
Mohamed Shein, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba,
Hamadi Bakari Mshindo, alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya Mkoa
wa Kusini Pemba, akiwa na ujumbe wake kupata taarifa ya kazi za mendeleo
ya Mkoa huo, alipoaanza ziara ya kuangalia miradi mbalimbali ya maendeleo.
Baadhi
ya Viongozi walioungana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, katika ziara Mkoa
wa Kusini Pemba, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Meja Mstaafu Juma Kasim
Tindwa (hayupo pichani), alipokuwa akisoma ripoti ya kazi za maendeleo, wakati
Rais alipoanza ziara hiyo, ya kuangalia maendeleo ya miradi mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa Meja Mstaafu Juma Kasim Tindwa, akisoma ripoti ya kazi za maendeleo kwa Mkoa wa Kusini Pemba, mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, alipoanza ziara hiyo kwa kupokea taarifa hiyo na kuweza kuangalia miradi mbali mbali ya maendeleo ndani ya shehia na wilaya za Mkoa wa Kusini Pemba leo.
Mawaziri
wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Viongozi wengine
walipokuwa wakisikiliza ripoti ya Kazi za maendeleo ya Mkoa wa
Kusini Pemba, iliyokuwa ikisomwa na Mkuu wa Mkoa huo, Meja mstaafu Juma Kassim
Tindwa(hayupo pichani), kabla ya kutembelea miradi mbali katika Wilaya ya Chake chake leo.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali
Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza na wakati wa kupokea taarifa
ya ripoti ya kazi za maendeleo ndani ya Mkoa wa Kusini Pemba leo, iliyoanza kwa wilaya ya Chake chake.
Baadhi
ya Wananchi na Viongozi waliohudhuria katika Mkutano
wa Utoaji wa taarifa ya ripoti ya kazi za maendeleo, kwa Mkoa wa
Kusini Pemba, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Meja Mstaafu Juma Kasim Tindwa (hayupo
pichani), akisoma ripoti hiyo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, alipoanza ziara hiyo ya kuangalia maendeleo ya miradi mbalimbali leo.
Mfanyakazi
wa Shirika la Umeme Pemba Shaibu Hassan, alipokuwa akitoa malalamiko
yake mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
Dk. Ali Mohamed Shein, kuhusu ubadhirifu Fedha ndani ya Shirika
hilo, wakati wa utoaji wa ripoti ya kazi za Mkoa wa Kusini Pemba, wakati
wa ziara ya kuangalia maendeleo ya miradi mbalimbali, ambayo ikiwemi iliyoanzishwa na wananchi.
No comments:
Post a Comment