TANGAZO


Tuesday, March 19, 2013

Kinana akutana na Mjumbe wa Kamati Kuu (CPC) China

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha China (PCP), Ai Ping, Kinana alipowasili kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Mambo ya Nje ya chama cha CPC, mjini Beijing, China, Machi 19, 2013. Kinana ambaye aliwasili kwenye Ofisi hizo na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM, wapo nchini China  kwa ajili ziara ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha CPC. (Picha na Bashir Nkoromo).

Katibu wa NEC ya CCM,  Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha China (PCP), Ai Ping, alipowasili na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Mambo ya Nje ya chama cha CPC, mjini Beijing, China, Machi 19, 2013. Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM, wapo nchini China  kwa ajili ziara ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha CPC. 


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) na ujumbe wake wakiwa kwenye semina kuhusu uzoefu wa China katika kupunguza umasikini  vijijini, semina hiyo iliendeshwa na Mkurugenzi wa  Kituo cha Kimataifa cha kupambana na umasikini, Profesa  Huang Chenwei (kushoto), katika hoteli ya Wanshou, Beijing, China, Machi 19, 2013. Wengine ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhisiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kulia), Kulia kwa Kinana ni, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi, Yusuf Yusuf na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu. Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM, wapo nchini China  kwa ajili ziara ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha CPC.


MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Ai Ping, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa China ( kulia) akiendesha semina kwa kuhusu ujenzi wa vyama vingi katika mazingira ya utandawazi, kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kushoto) na ujumbe wake wa viongozi 14 wa CCM, leo Machi 19, 2013. Semina hiyo ilifanyika katika Ofisi za Mambo ya Nje ya Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC). Viongozi wa CCM kutoka kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro. Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi, Yusuf Mohamed Yusuf, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu, Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine Shigela na Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi.  Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM, wapo nchini China  kwa ajili ziara ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha CPC. 


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Siasa na Uhisiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, wakibadilishana mawazo, baada ya semina kuhusu uzoefu wa China katika kupunguza umasikini, iliendeshwa na Mkurugenzi wa  Kituo cha Kimataifa cha kupambana na umasikini, Profesa  Huang Chenwei, katika hoteli ya Wanshou, Beijing, China, Machi 19, 2013. Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM, wapo nchini China  kwa ajili ziara ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha CPC. 

No comments:

Post a Comment