TANGAZO


Saturday, March 16, 2013

Yanga yaichapa Ruvu Shooting bao 1-0, Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa

 Nizar Khalfan wa Yanga (kulia), akipambana na Hassan Dilunga wa Ruvu Shootinga, wakati timu hizo zilipopambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni. Katika mchezo huo, Yanga imeshinda bao 1-0.
Hassan Dilunga wa Ruvu Shootinga, akimtoka Nizar Khalfan wa Yanga katika mchezo huo. 

Nizar Khalfan wa Yanga akipambana na Michael Aidan wa Ruvu (aliyedondoka chini) katika mchezo huo.
Simon Msuva wa Yanga, akijaribu kumpiga chenga Gideon Tepo wa Ruvu Shootinga katika mchezo huo.
Simon Msuva wa Yanga, akijaribu kumuhadaa Gideon Tepo wa Ruvu Shootinga katika mchezo huo.
Gideon Tepo wa Ruvu Shootinga, akitolewa nje na vijana wa huduma ya kwanza baada ya kuumia wakati akiwania mpira katika mchezo huo. 
Gideon Tepo wa Ruvu Shootinga, akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kuumia wakati akiwania mpira katika mchezo huo. 

Mashabiki wa Yanga wakifuatilia mchezo kati ya timu yao na Ruvu Shootinga, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.
Mashabiki wa Yanga wakishangilia timu yao ilipopambana na Ruvu Shootinga, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.
 Hamis Kiiza wa Yanga akimtoka Ibrahim Shaaban wa Ruvu Shooting.
 Wachezaji wa Ruvu Shhoting, wakipambana na David Luhende wa Yanga katika mchezo huo.
 Hadi mwisho wa mchezo huo, ubao wa matangazo ulikuwa ukisomeka Yanga bao 1, Ruvu Shooting o.
David Luhende wa Yanga, akimtoka mmoja wa wachezaji wa Ruvu Shooting.

No comments:

Post a Comment