Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki, Dk. Salim Ahmed Salim (kulia), Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (kushoto) na Mwenyekiti Mtendaji wa hospitali hiyo pamoja na Chuo hicho, Kokushubira Kairuki.
Viongozi wa Dini waliohudhuria hafla hiyo, kutoka kulia ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa.
Mwenyekiti Mtendaji wa Hospitali na Chuo Kikuu cha Hubert Kairuki, Kokushubira Kairuki, akitoa neno la shukurani kwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, Rais Jakaya Kikwete.
Mama mzazi wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Hospitali na Chuo cha Hubert Kiruki, marehemu Profesa Dk. Hubert Kairuki (katikati), akisaidiwa kutembea wakati akienda kupiga picha ya pamoja na Rais Jakaya Kikwete.
Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Donan Mmbando (kushoto), akiwa katika hafla hiyo.
Wafanyakazi wa Hospitali hiyo na wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Hospitali hiyo, wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi, Rais Jakaya Kikwete.
Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali hiyo na wageni waalikwa wakiwa katika maadhimisho hayo.
Sir George Kahama (kushoto) na wageni wengine waalikwa wakiwa kwenye sherehe hizo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali hiyo, wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye maadhimisho hayo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali hiyo, wakiwa katika maadhimisho hayo, jijini leo.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Rais Jakaya Kikwete, akihutubia wafanyakazi pamoja na wageni mbalimbali waalikwa. Kulia ni Rais msataafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik.
Wafanyakazi pamoja na wageni waalikwa wakiwa kwenye sherehe hizo.
Wageni waalikwa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wakiwa kwenye sherehe hizo.
Hosteli mpya kwa ajili ya wanafunzi wa Chuo cha Tiba cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki, iliyofunguliwa na Rais Kikwete inavyoonekana katika picha.
Mchungaji wa Kanisa la Asemblies of God (katikati), akisaidiwa kutembea kwenda kupiga picha ya pamoja na Rais Jakaya Kikwete, Mchungaji huyo pamoja na viongozi wa Kanisa hilo, walikubali kuwa wadhamini wa Hospitali hiyo, kufuatia utaratibu wa Serikali kuwa Hospitali zote ziwe na udhamini wa taasisi za dini na si mtu binafsi.
Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali pamoja na wanafamilia wa marehemu Profesa Dk. Hubert Kairuki.
Rais Jakaya Kikwete, akifungua pazia kuashiria ufunguzi wa Hosteli ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki, wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 25 ya utoaji wa huduma ya afya tangu kuanzishwa kwa Hospitali ya Hubert Kairuki mwaka 1987-2012, iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Hospitali hiyo pamoja na Chuo, Kokushubira Kairuki.
Rais Kikwete akimpa mkono wa pongezi, Atlay Thawe pamoja na pacha mwenzake ni miongoni mwa vijana waliozaliwa katika hospitali hiyo, zaidi ya miaka 20 iliyopita.
Rais Jakaya Kikwete, akipeana mkono na Mwenyekiti Mtendaji wa Hospitali hiyo pamoja na Chuo chake, Kokushubira Kairuki baada ya kukabidhiwa tuzo na Uongozi wa Hospitali hiyo kwa mchango wake katika sekta ya Afya hasa katika kuisaidia Hospitali hiyo.
Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi tuzo mmoja kati vijana waliozaliwa katika hospitali hiyo.
Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi (kushoto), akiteta jambo na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid wakati wakisubiri kuwasili kwa mgeni rasmi Rais Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete, akipatiwa maelekezo na Mkurugenzi wa Hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki, Assey Mchomvu (kulia), wakati akiangalia moja ya mfano wa Jengo la Hospitali hiyo.
Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi tuzo Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi iliyotolewa na Hospitali hiyo, ikiwa ni katika kutoa shukurani kwake kutokana na mchango wake katika sekta ya afya na kutoa kibali cha kupata eneo hilo, ilipojengwa Hospitali hiyo, wakati wa uongozi wake. (Picha zote kwa hisani ya Habari za jamii blog)
No comments:
Post a Comment