TANGAZO


Sunday, March 17, 2013

Katibu Mkuu wa CCM, Abdurrahaman Kinana awasili Beijing nchini China

"KARIBU BEIJING", Balozi wa Tanzania nchini China, Philip Marmo (kulia), anaelekea kumweleza Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Abdurrahman Kinana, wakati alipokuwa akizungumza naye kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing, nchini China, baada ya Kinana na ujumbe wake kuwasili akitokea jimbo la Sichuani leo, Machi 17, 2013. Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM, wapo nchini china kwa ziara ya siku kumi ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China. (Picha zote na Bashir Nkoromo).

Balozi wa Tanzania nchini China, Philip Marmo akizungumza baada ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdurrahman Kinana na ujumbe wake, nyumbani kwake, kwenye Ubalozi wa Tanzania, mjini Beijing, China, baada ya kuwasili leo Machi 17, 2013, akitokea jimbo la Sichuan.  Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM wapo nchini China kwa ziara ya siku kumi ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai. 

Katibu Mkuu wa CCM, Abdurrahman Kinana akizungumza, nyumbani kwa Balozi wa Tanzania mjini Beijing, China, Philip Marmo (wapili kushoto), baada ya kuwasili leo, Machi 17, 2013 akitokea Sichuan. Kinana na Ujumbe wa viongozi 14 wa CCM yupo nchini China tangu Machi 11, mwaka huu, akiwa katika ziara ya mafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali Vuai na Kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,  Khadija  Aboud.

Baadhi ya Watanzania waliopo jijini Beijing, China wakichangamkia kupigapicha na Katibu wa NEC, Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (wa tatu kulia), nyumbani kwa Balozi wa Tanzania nchini China leo.

Baadhi ya Watanzania wanaoishi Beijing, wakimlaki Katibu Mkuu wa CCM, Kinana na msafara wake, nyumbani kwa Balozi Marmo, Beijing China, leo Machi 17, 2013. Kulia ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Beijing, Daninga Daniel.


Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mbunge wa Busega, Dk. Titus Kamani akiwasalimia baadhi ya Watanzania wanaoishi Beijing China, baada ya kuwasili na Katibu Mkuu wa CCM, Abdurrahman Kinana, nyumbani kwa Balozi wa Tanzania nchini China, Philp Marmo leo, Machi 17, 2013. Kamani ni miongoni mwa viongozi 14 wa CCM, waliopo katika msafara wa Kinana ambaye yupo nchini China na ujumbe huo kwa ziara ya kikazi, kufuatia mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China.

No comments:

Post a Comment