Mataifa yanayoimarika zaidi kiuchumi duniani yanakutana Afrika Kusini katika mji wa Durban ambapo yanajadiliana maswala mbalimbali yanayohusiana na uundaji wa Benki ya pamoja ya ustawi kupingana na Benki ya Dunia na shirika la Fedha la dunia IMF.
Viongozi wa Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini, yanayojulikana kama BRICS, yatagusia mbinu za kuimarisha uchumi, ambao umedorora katika mataifa yote hayo wanachama.
Kabla ya mashauriano hayo, Uchina na Brazil, walikubaliana kubadilisha biashara kati yao ya jumla ya Dola Bilioni 30 kwa sarafu zao badala ya kutumia Dola ya Marekani.
No comments:
Post a Comment