TANGAZO


Tuesday, March 26, 2013

Korea Kusini yaonya Kaskazini kuhusu siasa zake



Rais Park Geun-Hye
Rais mpya wa Korea Kusini , Park Geun-Hye, amehimiza Korea Kaskazini kubadilisha mkondo wake wa siasa zake ili kutuliza uhasama unaoendelea kukuwa kati ya mataifa hayo mawili.
Katika ilani yake ya hivi karibuni Korea Kaskazini imesema kuwa imelenga makombora yake ya masafa marefu na yale ya kawaida ili yaweze kuvamia vituo vya Marekani vilivyo Bahari ya Pacific wakati wowote.
Taifa hilo la Kaskazini limeimarisha vitisho vyake kama hatua ya kujibu mazoezi makali ya kivita yanayondeshwa na Korea Kusini kwa ushirikiano na Marekani na pia kwa vikwazo vilivyowekewa dhidi ya taifa hilo katika hatua ya kulizika kuimarisha zana zake za kinukilia.
Akiongea katika hafla ya kuadhimisha kuzamishwa kwa meli ya Korea Kusini miaka mitatu iliyopita, Bi Park alisema matumaini yaliyopo kwa Korea Kaskazini ni kupuuza silaha zake za kinukilia na makombora yake.

No comments:

Post a Comment