Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu akiwaonesha jambo baadhi ya viongozi wa Kata ya Ilala na Serikali ya mtaa wa Sharif Shamba, wakati alipokuwa akikagua uchafuzi wa mazingira ya Mfereji wa Buguruni Malapa, unaotoka Barabara ya Nyerere hadi Bonde la Msimbazi, jijini Dar es Salaam juzi. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu akiongozana na baadhi ya viongozi wa Kata ya Ilala na Serikali ya Mtaa wa Sharif Shamba, kukagua uchafuzi wa mazingira ya Mfereji wa Buguruni Malapa, unaotoka Barabara ya Nyerere hadi Bonde la Msimbazi, jijini Dar es Salaam juzi.
Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu akiwaangalia wananchi waliokuwa wakivuka mfereji huo, kutoka Saharif Shamba kuelekea Buguruni Malapa huku maji taka yakiwa yamezagaa sehemu ya mtaro huo, uliomomonyoka kutokana na mvua zinazonyesha.
Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu akijaribu kuvuka mfereji huo, kutoka eneo la Saharif Shamba kuelekea Buguruni Malapa huku maji taka yakiwa yamezagaa sehemu ya mtaro huo, uliomomonyoka kutokana na mvua zinazonyesha.
Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu akiwaangalia wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Msimbazi wakati wakivuka kwenye mtaro huo, kuelekea shuleni kwao, Msimbazi Centre, wakitokea Buguruni wanakoishi.
Sehemu ya Mtaro huo, maeneo ya Sharif Shamba, inavyoonekana baada ya uchafunzi huo wa mazingira na mmomonyoko wa kingo za mfereji huo.
No comments:
Post a Comment