Rais wa China, Xi Jinping akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete funguo, ikiwa ni ishara ya kukabidhi rasmi Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam jana. Kituo hicho kimejengwa kwa msaada wa Serikali ya China kwa gharama ya Dola za Marekani mil. 15.
Rais Kikwete akifurahia funguo hiyo aliyokabidhiwa na Rais wa China, Xi Jinping.
Rais wa China, Xi Jinping (kushoto), akiangalia simba aliyekaushwa muda mfupi kabla ya Rais Jakaya Kikwete kumpatia zawadi hiyo, Ikulu, Dar es Salaam jana usiku.
Rais wa China, Xi Jinping (kushoto), akiangalia simba aliyekaushwa muda mfupi kabla ya Rais Jakaya Kikwete kumpatia zawadi hiyo, Ikulu, Dar es Salaam jana usiku.
Rais wa China, Xi Jinping (kushoto), akihutubia jana kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam, kuhusu sera ya nchi hiyo kwa nchi za Afrika. Kituo hicho cha kisasa kimejengwa kwa msaada wa Serikali ya China kwa gharama ya dola za Marekani mil. 15.
Baadhi ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika hafla ya kukabidhi Kituo hicho cha Kimataifa, wakisikiliza hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa China, Xi Jinping.
Rais wa China, Xi Jinping, akisalimiana na Waziri wa Fedhawa Zanzibar, Omar Yussuf Mzee. Katikati ni Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Rais wa China, Xi Jinping, akizungumza na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, wakati alipokutana naye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam jana katika ziara yake ya siku mbili nchini.
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na ujumbe wake, akizunguma na Rais wa China, Xi Jinpinga, wakati alipokutana naye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam jana.
Rais wa China, Xi Jinpinga, akiwa na ujumbe wake, akizunguma na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, wakati alipokutana naye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam jana katika ziara yake ya siku mbili nchini.
Rais wa Awamu ya Tatu wa Tanzania, Benjamin Mkapa (kushoto) akisalimiana na Rais wa China, Xi Jinping na baadaye kufanya naye mazungumzo Dar es Salaam jana.
Rais wa China, Xi Jinping, akiwa na ujumbe wake, akizungumza na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana, wakati wa ziara yake ya siku mbili nchini.
Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, akiwa na ujumbe wake, akizungumza na Rais wa China, Xi Jinping, Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana, wakati wa ziara ya Rais huyo nchini.
Rais Jakaya Kikwete akiwa na mgeni wake, Rais wa China, Xi Jinping, wakiwasili kwenye makaburi ya Wataalamu wa Kichina, Majohe, Dar es Salaam jana, waliokufa wakati wa shughuli mbalimbali za ujenzi wa taifa nchini.
Wakitoa heshima zao kwenye makaburi hayo.
Ujumbe aliofuatana nao ukiwa kwenye hafla hiyo, makaburini hapo jana.
Rais Kikwete, akiwa na mgeni wake, Rais wa China, Rais Xi Jianping (kushoto) na mkewe Liyuan akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo cha makaburi hayo, huku akiangaliwa na mke wake, Mama Salma.
Rais wa China, Rais Xi Jianping (kushoto) na mkewe Liyuan akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo cha makaburi hayo, huku akiangaliwa na mwenyeji wake, Rais Kikwete na mke wake, Mama Salma (kulia), wakati wa hafla hiyo.
Rais Jakaya Kikwete, akihutubia kwenye makaburi hayo, kuelezea masikitiko yake kutokana na vifo vya wananchi wa China wakati wa ujenzi wa shughuli mbalimbali za Kitaifa, nchini.
Rais wa China, Xin Jianpig, akihtubia wakati wa hafla hiyo makaburi hapo jana.
Rais Jakaya Kikwete na mgeni wake, Rais wa China, Xi Jinping na wake zao wakiangalia ngoma ya Msewe ya wenyeji wa Pemba katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam juzi, wakati Rais huyo akiondoka nchini baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili.
Rais wa China, Xi jinpiga, akizungumza na Balozi wa nchi hiyo, nchini pamoja na mkewe, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Rais wa China, Xi Jinping, akitambulishwa kwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Taifa, Dk. Asha Rose Migiro, wakati akiwa tayari Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa safari ya Afrika Kusini jana.
Rais wa China, Xi Jinping akisalimiana na kuagana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdurrahaman Kinana, Uwanjani hapo jana.
Rais Jakaya Kikwete, akiagana na mgeni wake, Rais wa China, Xi Jinping, wakati akiondoka nchini kuelekea nchini kuelekea Afrika Kusini jana.
Rais wa China, akiagana na mke wa Rais Kikwete, Mama Salma wakati akiondoka kuelekea nchini Afrika Kusini jana.
Wake wa Rais Salma Kikwete na wa Rais wa China Liyuan , wakiagana kabla ya kupanda ndege, kuelekea Afrika Kusini, Dar es Salaam jana.
Watanzania wakipunga bendera kumuaga Rais wa China, mkewe pamoja na Ujumbe wake, wakati wakiondoka nchini kuelekea Afrika Kusini.
Rais Jakaya Kikwete, akiwa na Makamu wake, Dk. Gharib Bilal (kushoto kwake), Balozi wa China na mkewe (kulia), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kulia kwa Rais) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadik, wakimuaga Rais wa China pamoja na ujumbe wake, wakati wakiondoka nchini kuelekea Afrika Kusini jana.
Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping na mkewe, Liyuan wakipunga mkono kuwaaga Watanzania waliokuwepo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, wakati wakiondoka kwenda Afrika Kusini jana.
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (wa pili kushoto), Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia), Katibu Mkuu wake, Injinia Omar Chambo (kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, John Mngodo (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Home Shopping Centre, Gharib Said Mohamed (kushoto kwa meya), wakiwa uwanjani hapo wakimuaga Rais huyo.
|
No comments:
Post a Comment