TANGAZO


Tuesday, March 26, 2013

Ntaganda afikishwa mahakamani ICC


Bosco Ntaganda mahakamani ICC

Mshukiwa wa uhalifu wa kivita nchini Congo Bosco Ntaganda amefikishwa katika mahakama ya kimataifa ya jinai huko The Hague na kusema hana hatia yeyote.
Lakini Ntaganda alikatizwa na Jaji ambaye aliyemuarifu kwamba hakutakiwa kujibu mashitaka wakati huu hadi kesi inayomkabili itakapoanza kusikilizwa rasmi.
Ntaganda anakabiliwa na mashitaka ya mauaji, ubakaji na kuwasajili watoto kilazima katika jeshi katika vita vya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Hicho ni kikao cha kwanza cha mbabe huyo tangu ajisalimishe kwa ubalozi wa Marekani mjini Kigali Rwanda, Jumatatu juma lililopita.
Jenerali Ntaganda amefahamishwa kuhusu mashtaka anayokabiliwa nayo na tarehe ambayo atatakiwa kufika mbele ya mahakama hiyo kwa kesi dhidi yake.
Anakabiliwa na makosa kumi ikiwemo ubakaji , mauaji na kuwatumia watoto kama wanajeshi.
Jenerali Ntaganda ni mshukiwa wa kwanza kujisalimisha kwa mahakama ya ICC kwa hiari.

Muaji

Alijikabidhi kwa ubalozi wa Marekani nchini Rwanda tarehe 17 Machi, na alisafirishwa kwa ndege nchini Uholanzi, makao makuu ya mahakama ya ICC.
Ntaganda alijulikana kama "The Terminator", na alipigania makundi kadhaa ya waasi na hata wakati mmoja alikuwa mwanajeshi katika jeshi la serikali ya DRC.
Hivi karibuni Ntaganda alijulikana kama mmoja wa viongozi wa kundi la waasi wa M23, ambalo limekuwa likipigana na serikali ya DRC Mashariki mwa nchi.
Harakati zake aliziendesha kati ya mwaka 2002-2003.
Ntaganda na kundi la waasi DRC
Siku ya Jumanne atatakiwa kuthibitisha ikiwa yeye ndiye Ntaganda na atatakiwa kuambia majaji lugha anayotaka kutumia wakati wa kesi yake.
Kisha mahakama itaamua siku ambayo kesi itasikilizwa kwa kikamilifu ambapo itaweza kubainika ikiwa kuna ushahidi wa kutosha kumfungulia mashtaka Ntaganda.
Mashariki mwa DRC imekumbwa na mgogoro wa muda wa mrefu ukihusishwa na ghasia za kikabila na uhasama wa makabila pamoja na ushindani wa rasilimali.
Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yamesifu sana hatua ya Ntaganda kujisalimisha na kuitaja kama ushindi kwa sheria ya kimataifa na waathiriwa uhalifu katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment