TANGAZO


Monday, March 25, 2013

Taifa Stars ilipoinyanyasa Morocco, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, yaipiga 3-1

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Morocco wakiimba wimbo wa Taifa wa nchi yao, kabla ya mchezo wa mchujo dhidi ya Taifa Stars, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana, kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia, nchini Brazili mwakani. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Kikosi cha timu ya Morocco kikipiga picha ya pamoja kabla ya mchezo huo dhidi ya Taifa Stars, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana. Mchezo huo, ulimalizika kwa Tanzania kuipa kichapo cha mabao 3-1.

 Wachezaji wa Taifa Stars wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya mchezo huo na Morocco, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana. 

 Kikosi cha Stars kikipigapicha ya kumbukumbu kabla ya kuanza kwa mchezo huo jana.


 Erasto Nyoni wa Stars (kushoto), akiwaniampira na Bergdichi Zakarya wa Morocco.


 Erasto Nyoni wa Stars (kushoto), ajaribu kumpiga chenga Bergdichi Zakarya wa Morocco, katika mchezo huo.

Shomari Kapombe wa Taifa Stars, akiwatoka Abourazouk Hamza (kushoto) na Bellakhar Nadir (16) wa Morocco

Mrisho Ngassa wa Stars akimtoka Eladoua Issam wa Morocco.

 Mbwana Samatta wa Stars akiudhibiti mpira uliokuwa ukiwaniwa na Bergdichi Zakarya wa Morocco.

 Mashabiki wa Taifa Stars, wakifuatilia mchezo huo.

Mashabiki wakifuatilia mchezo huo kwa makini.

Thomas Ulimwengu wa Taifa Stars, akijaribu kuudhibiti mpira miguuni mwa Eladoua Issam wa Morocco.
Thomas Ulimwengu wa Taifa Stars, akijaribu kumnyang'anya mpira Achchakir Abderrahim wa Taifa ya Morocco.

Thomas Ulimwengu wa Taifa Stars, akipigwa kikumbo na Achchakir Abderrahim wa Taifa ya Morocco katika mchezo huo.

Thomas Ulimwengu wa Taifa Stars, akimzidi nguvu Achchakir Abderrahim wa Taifa ya Morocco wakati akijaribu kumnyang'anya mpira miguuni mwake katika mchezo huo.

Mbwana Samatta wa Stars akishangilia bao lake, aliloifungia Stars likiwa ni bao la pili kwa Stars baada ya la kwanza kuwekwa kimiani na pacha wake, wanayecheza pamoja TP Mazembe ya DRC, Zaire, huku Salum Abubakar (kulia) na Amri Kiemba wakimfuata nyuma yake.

Thomas Ulimwengu wa Taifa Satrs, akipiga mpira mbele huku akifuatwa na Hafid Abdelillah wa Morocco.



Thomas Ulimwengu wa Taifa Satrs, akipambana na Achchakir Abderrahim wa Taifa ya Morocco katika mchezo huo.


 Mbwana Samatta akifunga goli lake la pili katika mchezo huo, ikiwa ni goli la tatu kwa Stars.

Mashabiki wa Stars wakishangilia bao hilo, lililowamaliza nguvu Wamorocco, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana.

Mbwana Samatta (katikati), Amri Kiemba (kushoto) na Thomas Ulimwengu, wote wa Stars wakishangilia goli la tatu la timu hiyo, lililofungwa na Samatta.

Mashabiki wa Stars wakishangilia goli hilo.

Hadi dakika ya 80 ya mchezo huo, ubao wa matangazo ulikuwa ukisomeka kama inavyoonekana pichani.



Eladoua Issam wa Morocco, akiudhibiti mpira uliokuwa ukiwaniwa na Thomas Ulimwengu wa Stars.

Thomas Ulimwengu wa Stars, akitolewa nje baada ya kuumia kifundo cha mguu wake wa kushoto.

Mbwana Samatta akihojiwa na mtangazaji wa BBC Swahili, Erick David Nampesya, mara baada ya kumalizika mchezo huo jana, ambapo Stars ilishinda mabao 3-i,  mawili kati ya hayo yakiwekwa kimiani na Samatta.

Hadi mwisho wa mchezo matokeo yalikuwa kama yanavyosomeka kwenye ubao wa matangazo, uwanjani hapo.

Mashabiki wa Stars wakiwa na furaha tele baada ya timu yao kuinyuka Morocco mabao 3-1.

Wachezaji wa Stars pamoja na viongozi na makocha wao wakiomba dua mara baada ya kumalizika mchezo huo, uwanjani hapo jana. 

No comments:

Post a Comment