Rais wa zamani wa Pakistan, Pervez Musharraf, amerudi Pakistan, baada ya kuishi uhamishoni kwa muda wa miaka minne.
Wanajeshi maalum waliojihami kikamilifu walimpokea katika uwanja wa ndege wa
Karachi, mara tu ndege iliyombeba kutoka Dubai ilipotua.
Jenerali Musharraf anatazamiwa kukiongoza chama chake katika uchaguzi mkuu wa mwezi Mei.
Huku hayo yakiendelea, wanajeshi 17 waliuawa katika shambulio la mtu aliyejilipua kwa mabomu katika eneo la kaskazini-magharibi mwa Pakistan.
Walishambuliwa katika kizuizi cha kuwakagua watu kaskazini mwa Waziristan, karibu na mpaka wa Afghanistan.
Eneo hilo linafahamika kuwa ni ngome ya wapiganaji wa Taliban na vile vile wale wa al-Qaeda.
Ukanda wa video hivi majuzi ulielezea namna walenga shabaha watampiga risasi Jenerali Musharraf, au hata kumshambulia kwa watu watakaojitoa mhanga kwa kujilipua kwa mabomu.
No comments:
Post a Comment