Maafisa wa utawala nchini Misri, wamewakamata wapigambizi
watatu waliokuwa wanajaribu kuukata mkonga wa internet ulio chini ya bahari.
Hata hivyo haikubainika ikiwa kupungua kwa kasi ya internet ilihusika moja kwa moja na kitendo cha watatu hao kuuharibi mkonga ijumaa iliyopita.
Wakati huo, kampuni inayomiliki mkonga huo, Seacom, ilisema kuwa mitandao kadhaa iliyounganisha Ulaya na Afrika , Mashariki ya kati na Asia ya Mashariki, iliathirika na hivyo kupunguza kasi ya huduma za internet.
Mkonga uliovamiwa Jumatano ulikuwa ule uliounganisha huduma za internet katika nchi za Asia mashariki na Ulaya Magharibi.
Uvamizi ulitokea umbali wa mita 750 Kaskazini mwa Alexandria.
Katika taarifa kwenye ukurasa wake wa Facebook Kanali Ali, alisema kuwa wapiga mbizi hao walikamatwa wakati wakivamia mkonga wa kampuni rasmi ya mawasiliano nchini Misri.
Hata hivyo hakutoa maelezo yoyote kuhusu nia ya wapiga mbizi hao.
No comments:
Post a Comment