Nzige wamevamia eneo kubwa la Madagascar na kutishia mimea
pamoja na kuzua wasiwasi kuhusu upungufu wa chakula.
Ni janga mbaya zaidi kuwahi kukumba kisiwa hicho tangu mwaka 1950, kwa mujibu wa FAO.
Mtaalamu wa kupambana na nzige, Annie Monard, aliambia BBC kuwa janga hilo ni tisho kubwa kwa kisiwa hicho cha bara hindi.
"janga la mwisho kama hili kuwahi kutokea ilikuwa miaka ya hamsini na kudumu kwa miaka 17 kwa hivyo ikiwa hakuna hatua zitakazochukuliwa basi huenda ikachukua miaka mitano au kumi kukamilika,'' alisema mtaalamu huyo.
Takriban asilimia 60,ya watu milioni 22 wa kisiwa hicho, huenda wakakumbwa na njaa.
Kwa sasa takriban nusu ya nchi imeathirika kutokana na nzige hao, kulingana na shirika la FAO.
Shirika hilo linataka, wahisani kuchangisha takriban dola milioni 22 kama msaada wa dharura kwa kufikia mwezi Juni ili kunyunyizia nzige hao dawa.
Janga hili la nzige limetishia mifugo na mchele shambani ambacho ni chakula rasmi cha raia wa Madagascar.
No comments:
Post a Comment