Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akimpatia Rais Jakaya Mrisho Kikwete, maelezo ya jinsi zoezi la uokoaji linavyoendelea katika eneo ambapo jengo la ghorofa 16, lilianguka na kufukia watu, Mtaa wa Indira Ghandhi karibu na makutano ya Barabara ya Morogoro, Dar es Salaam leo. Kulia ni Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akimpatia Rais Jakaya Mrisho Kikwete, maelezo ya jinsi zoezi la uokoaji linavyoendelea katika eneo ambapo jengo la ghorofa 16, lilianguka na kufukia watu, Mtaa wa Indira Ghandhi karibu na makutano ya Barabara ya Morogoro, Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi. (Picha na Freddy Maro)
Baadhi ya nondo zilizotumika kujengea jengo hilo, zikionekana zikiwa katika kiwango cha chini kabisa kisichoweza kuhili zege la jengo la ghorofa 16.
Kijiko kikiendelea leo kuondoa kifusi cha jengo hilo lililoporomoka.
Waokoaji wa kiondoa kifusi kwa kutumia majembe ya mkono.
Baadhi ya waokoaji wakiendelea kuondoa kifusi kwa kutumia majembe ya mkono.
Mwanajumuiya ya Shia, Ithnasheri Jamaat, ambapo jengo hilo lipo karibu na Msikiti wa Jumuiya hiyo, Ibrahim Raza, akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu athari za majengo marefu kama hayo, ambayo mkandarasi aliruhusiwa kujenga ghorofa 12 tu lakini akaongeza hadi kufikia 16.
Waokoaji wakikata nondo ili kuruhusu kuondolewa kifusi cha jengo hilo.
Kijiko kikivuta mabaki ya kuta pamoja na nondo zilizokuwa zimeshikana na zege la jengo hilo jijini leo.
Baadhi ya Askari Polisi, Jeshi la Wananchi (JWTZ) na wasamaria wema wakisubiri kusaidia kuokoa watu pamoja na mali zilizofukiwa kwenye kifusi cha jengo hilo leo.
Kijiko kikishusha kifusi na kukisawazisha ili kuwa rahisi kuondolewa na magari ya kuondoa kifusi.
Kikosi cha Zimamoto, wakimwagia maji huku kijiko kikiendelea kushusha kifusi cha jengo hilo leo, ikiwa ni siku ya pili ya uokoaji wa watu waliofukiwa pamoja na mali nyingine.
Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Jeshi la Wananchi (JWTZ) na watu wengine wakisubiri kuingia kazini kuondoa kifusi cha jengo hilo leo.
Kikosi cha Zimamoto, kikimwaga maji kwenye kifusi kwa ajili ya kupunguza vumbi na kutoa urahisi kwa kijiko kuondoa na kushusha kifusi hicho.
Mtaa wa Indira Gadhi lilipoporomoka jengo hilo, unavyoonekana wakati wa harakati za kuokoa na kuondoa kifusi hicho leo.
Magari ya kampuni ya Ujenzi, inayojenga Barabara ya Morogoro, Strobag, zikisubiri kubeba kifusi cha jengo hilo na kukipeleka Jangwani.
Moja ya gari lililoathirika na kuanguka kwa jengo hilo jana, likiwa katika maeneo ya tukio hilo leo.
Kijiko kikipakia kifusi cha jengo hilo kwenye magari ya kubebea kifusi na mchanga.
Kijiko kikipakia kifusi cha jengo hilo, kwenye magari ya kubebea kifusi na mchanga la Kampuni ya Ujenzi ya Strobag leo.
Kijiko kikiporomosha kifusi cha jengo hilo.
Kijiko kikiendelea kusomba kifusi cha jengo hilo na kukipakia kwenye malori ya kubebea leo jioni.
No comments:
Post a Comment