Mtalaamu wa Kitengo cha damu salama cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Mkude akimtoa damu Abubakari Mwankenja, wakati wanajumuiya ya Akhlaqul-Islaam (JAI), walipofika hospitalini hapo, kutoa damu kwa ajili ya hospitali hiyo pamoja na Taasisi ya MOI, Dar es Salaam leo. Nyuma ni baadhi ya wanajumuiya hiyo, wakiwa wamejipanga foleni, wakisubiri zamu yao ya kutoa damu. (Picha zote na Khamisi Mussa)
Mwanajumuiya hiyo, Fatuma Mussa (kulia), akitolewa damu na mtalaamu wa kitengo cha damu salama, Kibuna Rashid.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Rashid Seif (kushoto), akiwa katika zoezi hilo.
Mwanajumuiya hiyo, akitolewa damu na mtalaamu wa kitengo cha damu salama, Mohamed Kadeshi.
Wafanyakazi wa Taasisi ya Mifupa (MOI), wakipeana tende wakati wa zoezi la utoaji damu. Kushoto ni Sanifa Mohamed.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Rashid Seif, akihutubia baada ya utoaji huo wa damu.
Baadhi ya wanajumuiya hiyo, wakisubiri kutoa zamu yao ya kutoa damu.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Rashid Seif (katikati mwenye shati la drafti), akiwa na viongozi wa Jumiya ya Akhlaqul-Islaam (JAI), baada ya kujitolea damu, Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Rashid Seif (katikati waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Jumuiya hiya, baada ya kujitolea damu, Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Rashid Seif (katikati waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Jumuiya hiya, baada ya kujitolea damu, Dar es Salaam leo.
Dk. Efesper Nkya wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Kitengo cha Damu Salama (kulia), akikabidhiwa risala na Mwenyekiti wa Wadhamini wa Jumuiya ya Akhlaqul-Islaam (JAI), Abdallah Saad katika hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment