TANGAZO


Sunday, March 31, 2013

Kenya shuwari kidogo


Kumetokea ghasia mjini Kisumu, Kenya, baada ya uamuzi wa mahakama makuu ya Kenya kuthibitisha kuwa Uhuru Kenyatta ndiye aliyeshinda uchaguzi wa rais wa Kenya.
Mahakimu wa Kenya
Watu wawili walipigwa risasi na kuuwawa katika mapambano baina ya polisi na waandamanaji waliokuwa wakirusha mawe.
Piya kulikuwa na mvutano katika mitaa ya Nairobi inayomuunga mkono Raila Odinga.
Mwandishi wa BBC anasema wakati Kenya inasherehekea Pasaka, piya inaonesha kuwa iko tayari kumaliza kipindi hiki cha wasi-wasi.
Waliotabiri ghasia kama za miaka mitano iliyopita, hadi sasa hazikutokea.
Maswala yoyote yaliyokuwako kuhusu namna uchaguzi ulivyoendeshwa yanagubikwa na hamu ya watu kutaka amani.
Uhuru Kenyatta ameahidi kuongoza nchi kwa niaba ya Wakenya wote.
Itabidi achanganye jukumu hilo pamoja na kesi yake katika Mahakama Makuu ya Kimataifa, ICC.
Atavyoshughulikia kesi hiyo, ndiyo itaamua uongozi wake utavyokuwa siku za usoni

No comments:

Post a Comment