Katibu Mkuu wa CCM, Abdurrahman
Kinana akisalimiana na Waziri anayeshughulikia mambo ya chama katika Chama Cha
Kikomunisti cha China, Wang Jiarui, alipokutana naye leo Machi 20, 2013, kwenye
Ofisi za CPC, mjini Beijing, China na kuwa na mazungumzo naye. Nyuma ya Kinana
ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai. (Picha zote na Bashir
Nkoromo).
Katibu Mkuu wa CCM Abdurrahman
Kinana (kulia) akitazama baadhi ya malighafi, alipotembelea kampuni ya Aluminum
ya China (CHINALCO), alipotembelea kiwanda hicho mjini Beijing, Machi 20, 2013.
Wapili kulia ni Rais wa Kampuni hiyo Xiong Weiping.
Katibu Mkuu
wa CCM, Abdurrahman Kinana, akizungumza na waziri anayeshughulikia masuala ya
chama wa Chama cha Kikomnisti cha China, Wang Jiarui, alipokutana naye leo Machi
20, 2013, kwenye Ofisi za CPC, mjini Beijing, China.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdurrahman
Kinana akitia saini kweneye kitabu maalum cha wageni, katika kampuni ya Aluminum
ya China (CHINALCO). Kushoto ni Rais wa Kampuni hiyo, Xiong Weiping na wapili
kushoto ni Katibu wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Khamis Suleiman
Dadi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdurrahman
Kinana na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo na uongozi wa CHINALCO, Kinana na
ujumbe huo walipotembelea kampuni hiyo wakiwa katika ziara ya mafunzo Beijing,
China.
Katibu Mkuu wa CCM,
Abdurrahman Kinana akimpa zwadi ya kinyagoo cha Kimakonde cha aina ya 'Ujamaa',
Rais wa kampuni ya Aluminum ya China (CHINALCO) kilichopo mjini Beijing, Xiong
Weiping, alipotembelea kampuni hiyo na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM ambao yupo
nao katika ziara ya mafunzo nchini China.
Katibu Mkuu wa CCM,
Abdurrahman Kinana akipewa zwadi ya pambo la Kichina, na Rais wa kampuni ya
Aluminum ya China (CHINALCO) kilichopo mjini Beijing, Xiong Weiping, Kinana
alipotembelea kampuni hiyo na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM ambao yupo nao katika
ziara ya mafunzo nchini China. Kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
No comments:
Post a Comment