Mtoto Maisamali Karim (6), ambaye ameokolewa kutoka
katika madrasa ya Msikiti wa Khoja, Shia Ithna Asheri, Jamaat, iliyoangukiwa na
jengo lenye ghorofa 16, lililopo katika mtaa wa Indira Gandhi karibu na makutano ya Barabara ya Morogoro, Dares Salaam leo.
Changamoto ya uokoaji ni
ngumu, lakini vikosi mbalimbali vya uokoaji vinaendelea na zoezi hilo, ili kunusuru maisha
ya watu waliofukiwa na kifusi cha jengo hilo.
Hizi nia aina ya nondo zilizojengewa jengo hilo, ambazo zinaonekana sio imara kuweza kuhimili ujenzi wa jengo la ghorofa nyingi kama hilo. Ipo haja ya mamlaka husika likatupia macho Kampuni za ujenzi na ujenzi wa majengo kama hayo, ili kuokoa maisha ya
wajenzi, watumiaji wa majengo hayo na hata wapita njia.
Askari Polisi, wakiimarisha ulinzi
wakati zoezi la uokoaji wa watu na mali waliofukiwa na kifusi cha jengo hilo, likiendelea.
Huku jitihada za kuwaokoa watu na mali, zikiendelea, kwa juu zinaonekana nondo
nyembamba zilizokuwa zimejengewa jengo hilo na kuacha maswali mengi miongoni mwa mashuhuda wa tukio
hilo.
Waokoaji wakiendelea na jitihada za kuwatoa watu walionasa kwenye kifusi cha jengo hilo.
Wasamaria wema wakiendelea na jitihada zao za kuwaokoa watu na mali zao.
Waokoaji wakifunga mnyororo gari dogo, aina ya Toyota pick up kwa ajili ya kusaidia kuvuta nondo na mapande ya kuta za jengo hilo.
Askari Polisi wakimwangalia mmoja wa watu walipata majeraha wakati wa uokozi wa watu walioangukiwa na jengo hilo.
|
Hiki ni sehemu ya kifusi cha jengo hilo, baada ya kuanguka leo. |
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, akisalimiana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi kwenye tukio hilo. |
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, akipatiwa maelezo na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova kwenye tukio hilo. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi |
Waziri wa Mambo ya Ndani,
Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam (CP), Suleima Kova kuhusu jengo la ghorofa 16
lililoanguka majira ya saa mbili asubuhi katika makutano ya mtaa wa Indira
Ghandi na Barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi. Katika ajali hiyo watu wawili wamekufa papo
hapo.
Waokoaji wakiendela na
kazi ya uokoaji kwenye kifusi cha jengo hilo, huku askari nao wakiimarisha ulinzi.
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam(CP), Suleima
Kova, akizungumza na waandishi wa habari kwenye tukio hilo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (CP), Suleima Kova
akiwa katika eneo la tukio, akizungumza na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi na Mbunge wa kuteuliwa na Rais, James
Mbatia. (Picha zote kwa hisani ya Habari Mseto Blog)
No comments:
Post a Comment