TANGAZO


Wednesday, March 20, 2013

Huduma ya NMB, Vodacom yavutia maelfu ya Watanzania


                                       
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam, Machi 19, 2013 

WIKI chache baada ya Benki ya NMB na Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom kuingia katika makubaliano ya kutoa huduma za kifedha kwa njia ya simu kupitia huduma ya  M-PESA, huduma hiyo imekuwa na muitikio mkubwa kutoka kwa wateja kiasi ya kuvuka  malengo ya watumiaji wake.

Wateja wa benki hiyo ya NMB na wale ambao si wateja wa benki hiyo sasa wanaweza kupata  huduma inayosaidia kuweka na  kuhamisha fedha moja kwa moja kutoka kwenye akaunti ya benki ya NMB hadi akaunti ya M-Pesa kupitia mawakala wanaotoa huduma za M-Pesa zaidi 40,000 waliopo nchini.
Wiki chache baada ya uzinduzi wa huduma hii, kiasi cha wateja zaidi ya 35,000 wameweza kunufaika na huduma hii ambayo inategemewa kuongezeka zaidi ya hapo.
 Afisa Mkuu wa Biashara wa M-Pesa, Bw.  Jacques Voogt, alisema kuwa “katika kipindi hiki kifupi tumeshuhudia muitikio mkubwa sana kwenye huduma hii ya kipekee ambapo wafanyakazi wetu wamekuwa wakiendelea kutoa huduma bora. 
Kampuni ya Vodacom imefurahi kuona kwamba watu wengi zaidi wanajiunga kutumia huduma hiyo kila siku, ambapo ni maendeleo ya awali tu yanayonesha kupanuka kwa huduma hii nchi nzima.”
Wakati wa matayarisho ya uzinduzi wa huduma hii, wateja waliolengwa ni zaidi ya 729,000 ambao tayari walijisajili na wanaoendelea kutumia huduma ya NMB Mobile. Lakini pia ilitarajia kutoa uwanja mpana kwa watu wengine ambao sio wateja wa NMB ila wale wanaotumia huduma ya M-Pesa.
Aliongeza kuwa baadae huduma hiyo itapatikana maeneo ya vijijini ambapo tofauti na wateja wa mijini, kuna njia mbadala chache za huduma ya kuhamisha fedha. 
Alisema kuwa huduma hiyo ni ya aina yake ambayo itawezesha mzunguko wa miamala baina ya wateja na benki kufanyika kwa urahisi na haraka jambo litakalosaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki sanjari na kuboresha hali ya maisha na uchumi kwa Watanzania.
“Huduma hii imelenga katika kutimiza dhamira ya kampuni ya Vodacom ya kuwezesha watanzania kukabiliana na changamoto na kuweza kuboresha maisha yao ya kila siku” alisema Voogt na kuongeza kuwa,
“Huu ni mfano mwingine unaonyesha ni jinsi gani Vodacom inavyoongeza utumiaji wa teknolojia ili kuboresha maisha ya kila moja wetu. 
Tunayofuraha kwamba tumefanikiwa kuzikabili changamoto ambazo hadi miaka michache iliyopita zilionekana ni kikwazo kikubwa kwa watanzania, ila kutokana na haya yaliyotokea inaonesha kuwa dhamira yetu ya kuwasaidia watanzania inatimia. Tunategemea kuwepo kwa uwiano sawia mara tutakapozindua huduma hii maeneo ya vijijini, hii ikiwa ni tafsiri ya mafanikio kwa wote,”alisema Bw.Voogt.
Kwa ushirikiano wa kampuni ya Vodacom na benki ya NMB, uanzishwaji wa huduma hiyo utasaidia kuhudumia mamilioni ya wateja watakaotumia huduma ya kampuni ya simu yenye mtandao mkubwa Tanzania na benki yenye mtandao mkubwa nchini.
Huduma hiyo itafanywa popote palipo na tawi la NMB kuweza kupata huduma ya M-PESA au kutuma fedha katika benki kwa gharama ya sh 1500.

No comments:

Post a Comment