TANGAZO


Wednesday, March 20, 2013

Mvua yasababisha maporomoko Brazil

 

Waokoaji Petropolis
Waokoaji Petropolis
Takriban watu 27 wamefariki baada ya ardhi kuporomoka mjini Petropolis, eneo la milimani kaskazini mwa Rio de Janeiro, Brazil, baada ya mvua kubwa kunyesha.
Maporomoko hayo ya ardhi yaliukumba mji wa Petropolis baada ya mto kufurika.
Kundi kutoka Brazilian National Force limetumwa eneoni ili kuwasaidia waokoaji.
Kwa sasa mji huo uko katika hali ya tahadhari kwa sababu mvua zaidi inategemewa. Shule zimefungwa na wakaazi wametahadhirishwa wabaki majumbani mwao.
Wapoteza makao
Inakisiwa kwamba takriban watu 50 wamepoteza makao.
Eneo linalozunguka Petropolis lilikumbwa na maporomoko mnamo 2011 ambapo watu 900 walifariki.
Mwandishi wa BBC, Julia Carneiro aliyeko Rio, anasema kwamba ahadi toka kwa vyombo vya dola kwamba watajenga mikakati ya kuzuia visa kama hivyo hazijafua dafu.

No comments:

Post a Comment