Kina Mama wa Kata ya Ndoro, Lindi Mjini, Amina Ali na Saida Ali, wakimzawadia kuku, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika leo, Februari 20, 2013 katika kata hiyo.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Mama Slama Kikwete, Kata ya Ndoro, Lindi mjini, wakishangilia wakati wa mkutano huo.
Mama Salma Kikwete, akimkabidhi kadi mmoja wa wanachama wapya waliojiunga na CCM wakati wa mkutano wake, uliofanyika Kata ya Ndoro, Lindi mjini leo.
Wasanii Karim Suleiman, ambaye ni mlemavu wa mguu na Mohamed Ali, wakionesha umahiri wao, wa kucheza Kiduku katika mkutano wa hadhara, uliofanywa na Mama Salma Kikwete, Kata ya Ndoro, Lindi mjini leo, Februari 20, 2013.
Baadhi ya wanachama wapya wa CCM, wakila kiapo baada ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, kuwakabidhi kadi katika mkutano wa hadhara, uliofanyika mtaa wa Matopeni, Lindi mjini leo, Feb 20, 2013. (Picha zote na Bashir Nkoromo).
No comments:
Post a Comment