TANGAZO


Wednesday, February 20, 2013

Mbunge wa Ilala Mussa Zungu aongoza makabidhiano ya kitanda cha kujifungulia Hospitali ya Amana

Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF), Kanda ya Ilala, Evans Musiba (kushoto), akimkabidhi kitanda cha kujifungulia, chenye thamani ya sh. milioni 3.5, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Meshack Shimwela, kilichotolewa na mfuko huo, Dar es Salaam leo. Wa pili kushoto, anayeshuhudia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Zungu na wa pili kulia ni Meneja Mwandamizi wa PPF, kanda hiyo, Mordgard Lumbanga. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF), Kanda ya Ilala, Evans Musiba akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi kitanda cha kujifungulia, chenye thamani ya sh. milioni 3.5, kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Meshack Shimwela (kulia), kilichotolewa na mfuko huo, Dar es Salaam leo. Wa pili kushoto ni Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu na wa pili kulia ni Mchungaji wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Dar es Salaam, Ilala, Father, John Solomon. 

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Meshack Shimwela, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam, mara baada ya kukabidhiwa kitanda cha kujifungulia akinamama hospitalini hapo na Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF), Kanda ya Ilala, Evans Musiba (hayupo pichani), jijini leo. Kushoto ni Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu.

Sheikh Abdulwakat akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo leo. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan Zungu.

Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan Zungu, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF), Kanda ya Ilala, Evans Musiba (kushoto), kukabidhi kitanda cha kujifungulia, chenye thamani ya sh. milioni 3.5, kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Meshack Shimwela (wa tatu kulia), kilichotolewa na mfuko huo, Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja Mwandamizi wa PPF, kanda hiyo, Mordgard Lumbanga. 

Mchungaji wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Dar es Salaam, Ilala, Father, John Solomon, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF), Kanda ya Ilala, Evans Musiba (hayupo pichani), kukabidhi kitanda cha kujifungulia, chenye thamani ya sh. milioni 3.5, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Meshack Shimwela (hayupo pichani), kilichotolewa na mfuko huo, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Zungu.

Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Zungu, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, mara baada ya Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF), Kanda ya Ilala, Evans Musiba (kushoto), kumkabidhi kitanda cha kujifungulia, chenye thamani ya sh. milioni 3.5, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Meshack Shimwela, (kulia), kilichotolewa na mfuko huo.

Mchungaji Japhet Kyara akikiombea kitanda cha kujifungulia, mara baada ya Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF), Kanda ya Ilala, Evans Musiba(wa tatu kushoto), kukabidhi kitanda cha kujifungulia, chenye thamani ya sh. milioni 3.5, kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Meshack Shimwela (wa tatu kulia), kilichotolewa na mfuko huo, Dar es Salaam leo. Wa nne kushoto) ni Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu. 

Baadhi ya Maofisa wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF), Kanda ya Ilala, wakiwa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Amana, Madiwani na watendaji wa Kata ya Ilala pamoja na Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu (wa tatu kushoto), mbele ya kitanda cha kujifungulia wazazi, kilichokabidhiwa na Meneja wa Mfuko  wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF), Kanda ya Ilala, Evans Musiba.

No comments:

Post a Comment