TANGAZO


Wednesday, February 20, 2013

Rais Mwai Kibaki wa Kenya awasili jijini Dar es Salaam kwa ziara ya siku mbili nchini

Rais wa Jamhuri ya Kenya, Emilio Mwai Kibaki, akiwasili  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere leo, jijini Dar es Slaam kwa ziara ya siku mbili na kupokewa na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete. (Picha na Aron Msigwa -MAELEZO)

Rais wa Jamhuri ya Kenya, Emilio Mwai Kibaki akiwa na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kuwasili leo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam kwa ziara ya siku mbili nchini.

Rais wa Jamhuri ya Kenya, Emilio Mwai Kibaki akipata ukaribisho wa burudani ya vikundi mbalimbali vya ngoma, wakati wa mapokezi yake, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo kwa ziara ya siku mbili nchini.
Sehemu ya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakishiriki katika mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Kenya leo, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment