TANGAZO


Wednesday, February 20, 2013

Rais Dk. Shein aongoza kuuaga mwili, mazishi ya Padri Mushi Zanzibar


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasalimia wananchi wakati alipofika katika Kanisa la Minara miwili, mjini Zanzibar kutoa salamu za mwisho kwa Padri Evarist Gabriel Mushi, aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasijuilikana Jumapili iliyopita. Marehemu Padri Mushi, amezikwa leo, kijijini Kitope, Wilaya ya Kaskazini B Unguja. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akitia saini kitabu cha maombolezi ya marehemu Padri Evarist Gabriel Mushi, kwenye Kanisa la Minara miwili, mjini Zanzibar leo, ambapo alifika kutoa salamu za mwisho kwa mwili wa Padri huyo, aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasijuilikana, Jumapili iliyopita na amezikwa leo, Kijiji cha Kitope, Wilaya ya Kaskazini B Unguja. Kushoto ni Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar, Augustino Shao.



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akitia saini kitabu cha maombolezi ya Padri Evarist Gabriel Mushi, katika Kanisa la Minara miwili Mjini Zanzibar leo, ambapo alifika kutoa salamu za mwisho kwa mwili wa Padri huyo, aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasijuilikana Jumapili iliyopita na amezikwa leo kijini Kitope, Wilaya ya Kaskazini B Unguja. 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto), akitoa salamu za mwisho kwa mwili wa marehemu Padri Evarest Mushi katika Kanisa la Minara miwili, mjini Zanzibar leo. Padri Gabriel Mushi, alifariki kwa kupigwa risasi na watu wasijuilikana Jumapili iliyopita na amezikwa leo, Kijiji cha Kitope, Wilaya ya Kaskazini B Unguja. Katikati ni Askofu wa Kanisa Katoliki
Jimbo la Zanzibar, Augustino Shao. 

Baadhi ya waumini wa Kanisa Katoliki,  wakiwa katika mazishi ya marehemu Padri Evaristus Gabriel  Mushi, aliyezikwa leo, katika Viwanja vya Kanisa Katoliki la Kitope, Wilaya ya Kaskazini B Unguja. Padri Mushi alifariki Jumapili iliyopita kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, (katikati) akifuatana na Askofu wa Kanisa  Katoliki Jimbo la Zanzibar, Augustino Shao, wakielekea katika mazishi ya Padri Evaristus Gabriel Mushi, aliyezikwa katika Viwanja vya Kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja.


Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Tanga Antony Banzi, akiongoza sala, wakati wa mazishi ya marehemu  Padri Evaristus Gabriel Mushi, aliyekufa kwa kupigwa risasi Jumapili iliyopita na kuzikwa leo, katika viwanja vya Kanisa la Kitope, Wilaya ya Kaskazini B, Unguja leo.


Vijana waumini wa Dini ya Kikristo, wakiteremsha jeneza lenye mwili wa marehemu Padri Evaristus Gabriel  Mushi, katika kaburi alilozikwa leo katika Viwanja vya Kanisa la Katoliki la Kitope, Wilaya ya Kaskazini B Unguja. Marehemu alifariki kwa kupigwa risasi Jumapili iliyopita na watu wasiojulikana.


Askofu wa Kanisa  Katoliki Jimbo la Zanzibar, Augustino Shao, akitia udongo katika kaburi la marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi, aliyezikwa leo katika Viwanja vya Kanisa Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja.


Rais wa Zanbzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein (katikati), akitia udongo  katika kaburi la Marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo  katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Emanuel Nchimbi, akitia udongo kwenye kaburi la marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi, wakati wa mazishi yake, yaliyofanyika leo  katika Viwanja vya Kanisa la Kitope, Wilaya ya Kaskazini B, Unguja.


Waumini wa Dini ya Kikiristo wa Kanisa Katoliki pamoja na wananchi mbalimbali, wakifukia kwa udongo katika kaburi la marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi, aliyezikwa leo,  katika Viwanja vya Kanisa Katoliki la Kitope, Wilaya ya Kaskazini B, Unguja.


Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadham Policap Kadinali Pengo, akiwa pamoja na Maaskofu wengine, wakichomeka msalaba katika kaburi la marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi, aliyezikwa leo katika Viwanja vya Kanisa Katoliki la Kitope, Wilaya ya Kaskazini B, Unguja. Padri Mushi alifariki Jumapili iliyopita kwa kupigwa risasi na watu wasiojukana.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi, wakati wa mazishi yake, yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Kanisa la Kitope, Wilaya ya Kaskazini B Unguja.



Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar.                                                                                         
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein leo, ameongoza maelfu ya wananchi katika mazishi ya Padri Evarist Mushi huko Kitope, Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

 Katika mazishi hayo, viongozi mbali mbali wa dini na serikali walihudhuria akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad, Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wawakilishi, Wabunge, viongozi wa vyama vya siasa kutoka Zanzibar na Tanzania Bara na wananchi kutoka maeneo mbali mbali.

Mapema asubuhi, Dk. Shein alitoa salamu za mwisho kwa Padri Evarist Mushi huko katika kanisa la Minaramiwili, mjini Zanzibar.

Katika Kanisa la Minaramiwili sala ya mazishi iliongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar-es-Salaam Muadhama Kadinali Policap Pengo na ibada ya mazishi huko Kitope iliongozwa na Mhashamu Baba Askofu Antoni Banzi ambaye ni Askofu wa Jimbo Katoliki Tanga.

Akitoa salamu za Serikali katika mazishi hayo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud alisema kuwa Serikali imesikitishwa sana na kifo cha kiongozi huyo wa dini na kwamba ni  msiba mkubwa kwa Taifa.

Waziri Aboud aliwaomba wanafamilia wa marehemu pamoja na waumini wa dini ya Kikiristo kuwa watulivu na wastahamilivu katika kipindi hichi kigumu cha maombolezo ya kiongozi huyo.

Alimuelezea Padri Mushi kuwa alikuwa kiongozi aliyehubiri upendo, umoja na amani miongoni mwa waumini na wananchi wote wa Zanzibar na kuhimiza maadili mema, hivyo kumuenzi kwa kumuombea maisha mema ya milele.

Nazo salamu za familia zilitolewa na Fransis Mushi na kutoa shukurani kwa niaba ya familia  kwa mashirikiano makubwa waliyoyapata katika msiba huo tokea siku ya tukio la mauaji ya Padri huyo hadi leo alipofikishwa kwenye nyumba yake ya milele.

Nae Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Zanzibar Agostino Shao alieleza kusikitishwa na msiba huo na kumuomea marehemu amani ya milele.

Padri Mushi alizaliwa Juni 15, 1957 katika kijiji cha Uru Kimanganuni, katika Mkoa wa  Kilimanjaro na baada ya kumaliza elimu ya juu ya Sekondari mwaka 1976, alijiunga na Seminari Kuu Kibosho ambako alipata elimu ya Falsafa kati ya mwaka 1978 na 1979.

Mwaka 1980 alijiunga na Seminari Kuu ya Mtakatifu Paulo, Kipalapala Mkoani Tabora alipopata elimu ya tauhidi (Theology) hadi mwaka 1982.

Mwaka 1984 alirudi Kipalapala Mkoani Tabora kuendelea na masomo na mwaka huo huo alipata Daraja la Ushemasi katika Parokia ya Bikira Maria wa Rosari Kitope Zanzibar.

Katika maisha yake ya Upadri alishika vyeo mbali mbali ikiwemo Paroko wa Parokia ya Bikira Maria wa Rozari Kitope mwaka 1985, Paroko wa Parokia ya Moyo safi wa Maria wa Wete Pemba na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Antoni wa Padua Machui.

Padre Mushi aliuwawa kwa kupigwa risasi Februari 17 huko Mtoni, nje kidogo ya mji wa Zanzibar na watu wasiojulikana.

No comments:

Post a Comment