TANGAZO


Tuesday, February 5, 2013

Ufunguzi wa Kikao kazi cha Maofisa Habari wa Serikali Mjini Dodoma

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, akifungua mkutano wa Maofisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Serikali mjini Dodoma jana. Pamoja na mambo mengine amewataka kufanya kazi kwa kuzingatia weledi na kutoa taarifa sahihi kwa umma mara kwa mara kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Serikali.
Maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Serikali, wakiwa katika picha ya pamoja naWaziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (wa tatu kushoto waliokaa), mara baada ya ufunguzi wa kikao kazi hicho,  mjini Dodoma jana.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sihaba Nkinga, akizungumza na Maofisa Mawasiliano wa Serikali wakati wa Kikao kazi hicho, mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene akiwasilisha mada kuhusu Mtazamo mpya wa Mawasiliano katika Vitengo vya Mawasiliano, serikalini, wakati wa kikao kazi cha Maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Serikali mjini Dodoma kilichofunguliwa na Waziri, Dk. Fenella Mukangara, mjini Dodoma jana.
Ofisa Habari wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali,  Sarah Reuben, akichangia moja ya mada katika kikao kazi cha Maofisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Serikali mjini Dodoma jana.
Maofisa Mawasiliano wa Serikali, wakiendelea na kikao kazi chao, kujadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi Mjini Dodoma mara baada ya kufunguliwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara jana.
Maofisa Mawasiliano wa Serikali, wakisikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye kikao kazi cha kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji kazi, Mjini Dodoma mara baada ya kufunguliwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara jana.
Mmiliki na muendeshaji wa mtandao wahabari na matukio wa Mjengwa Blog kutoka Iringa, Majjid Mjengwa, akitoa mada kwa Maofisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Serikali, kuhusu Faida na Changamoto za Matumizi ya Mitandao ya Kijamii kwa Mawasiliano Serikalini, mjini Dodoma jana. (Picha zote na Aron Msigwa – MAELEZO)

No comments:

Post a Comment