TANGAZO


Tuesday, February 5, 2013

Rais Dk. Shein akabidhi Kombe la michuano ya Dk. Shein Cup, Uwanja wa Amani mjini Zanzibar

Mashabiki wa timu ya Kaskazini Unguja CCM,wakishangilia wakati timu ya CCM, Mkoa wa Mjini, walipoifunga goli la tatu katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Dk. Shein, mchezo, uliofanyika leo, Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, katika kilele cha miaka 36, ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).  Mgeni rasmi katika mchezo huo, alikuwa  Makamo Mwenyekiti wa Chama hicho, Visiwani, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein. Kaskazini iliibuka na ushindi wa mabao 3-1. (Picha zote na Ramadhan Othman Ikulu)
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na waamuzi wa Pambano la Fainali kati ya timu za Kaskazini Unguja na Mjini CCM, kabla ya mchezo   huo wa Dk. Shein Cup, uliochezwa Uwanja wa Amaan, mjini Zanzibar leo. Kaskazini iliweza kuicharaza Mjini kwa mabao 3-1, na kuibuka na hivyo kulinyakua kombe hilo, wakati wa kilele cha miaka 36 ya kuzaliwa CCM leo.
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na wachezaji wa  timu ya Kaskazini Unguja, kabla ya pambano lao na CCM, Mjini Magharibi katika mchezo wa fainali ya Dk. Shein Cup, Uwanja wa Amaan, Mjini Unguja leo, katika kilele cha mika 36 ya kuzaliwa CCM. 
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na wachezaji wa timu ya CCM, Mjini Magharibi wakati wa pambano lao na CCM Kaskazini, Unguja katika pambano la fainali ya Dk. Shein Cup, Uwanja wa Amaan, Mjini Unguja leo, ikiwa ni katika kilele cha maadhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa CCM. 
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya mashindano ya Dk. Shein Cup, kabla ya mpambano  wa fainali ya kombe hilo, uliochezwa leo Uwanja wa Amaan mjini Unguja.  Timu za CCM, Kaskazini Unguja na Mjini Magharibi zipambana katika fainali hizo, amazo zilikiwa ni katika kilele cha miaka 36 ya kuzaliwa CCM.
Mashabiki wa timu ya Mjini, wakishangilia wakati timu ya
CCM Mkoa mjini wakicheza na Timu ya Kaskazini katika mchezo wa fainali ya Dk. Shein Cup, mchezo uliofanyika leo Uwanja wa Amaan, mjini Unguja, wakati wa kilele cha miaka 36 ya kuzaliwa CCM. Katika mchezo huo, mgeni rasmi alikuwa Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein.
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Kombe la michuano ya Dk. Shein Cup, nahodha wa timu ya CCM, Kaskazini Unguja, Ali Hassan, baada ya timu yake kuibuka kidedea dhidi ya CCM Mjini kwa mabao 3-1, Uwanja wa Amaan, mjini Unguja leo katika kilele cha mika 36 ya kuzaliwa CCM.

No comments:

Post a Comment