TANGAZO


Tuesday, February 5, 2013

Timu ya Taifa ya Cameroon yatua Dar, waongea na waandishi wa habari

Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam leo, kuhusu mchezo wa kirafiki wa Kimataifa kati ya timu hiyo na ya Cameroon, utakaopigwa kesho, Februari 6, 2013. (Picha zote na Dande Junior wa Habari Mseto Blog)
Nahodha wa Taifa Stars, Juma Kaseja akizungumza kuhusu wachezaji wanavyouchukulia mpambano kati ya timu hizo, unaopigwa kesho, Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, wakati alikuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.


Meneja wa timu ya Cameroon, Rigobert Song (katikati), akiingia katika Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo.
Kocha wa timu ya Taifa ya Cameroon, Jean Paul akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu mpambano wao na Taifa Stars kesho, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa timu hiyo, Rigobert Song na nahodha wa timu hiyo, Wome Pierre.
Meneja wa timu hiyo, Rigobert Song akizungumza jambo na waandishi wa habari katika mkutano huo jijini leo. Katikati ni Kocha Mkuu wa timu hiyo, Jean Paul na Nahodha wake, Wome Pierre.
Meneja wa timu hiyo, Rigobert Song akifafanua jambo wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari leo. Katikati ni kocha Mkuu wa timu hiyo, Jean Paul na Nahodha, Wome Pierre.

No comments:

Post a Comment